the guardian 17
JF-Expert Member
- Aug 15, 2024
- 395
- 570
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda amesema Serikali ya Jamhuri ya Muumhano wa Tanzania inalitambua na kuthamini mchango wa Walinzi wa Jadi (Sungusungu) na kuwataka pia kufanya kazi kwa kuzingatia haki, kanuni na sheria za nchi.
Mkuu wa Mkoa ameyasema hayo leo Februari 20, 2025 kwa nyakati tofauti tofauti alipokuwa akizungumza na Sungusungu Wilayani Kwimba ambapo amesema ameamua kufanya ziara hiyo maalumu kwa lengo la kuona shughuli zinazofanywa na jeshi hilo la jadi.
Aidha, Mkuu wa Mkoa amelipongeza jeshi hilo kwa kuwa walinzi imara wa raia na mali zao lakini kubwa zaidi kwa kusaidia pia katika ulinzi wa mifugo ambapo kwa kiasi kikubwa wizi wa mifugo kwa maeneo ya vijijini umepungua kutokana na uimara wa Sungusungu.