RC Mtanda asema Serikali inatambua na kuthamini mchango wa Sungusungu

the guardian 17

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2024
Posts
395
Reaction score
570
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda amesema Serikali ya Jamhuri ya Muumhano wa Tanzania inalitambua na kuthamini mchango wa Walinzi wa Jadi (Sungusungu) na kuwataka pia kufanya kazi kwa kuzingatia haki, kanuni na sheria za nchi.

Mkuu wa Mkoa ameyasema hayo leo Februari 20, 2025 kwa nyakati tofauti tofauti alipokuwa akizungumza na Sungusungu Wilayani Kwimba ambapo amesema ameamua kufanya ziara hiyo maalumu kwa lengo la kuona shughuli zinazofanywa na jeshi hilo la jadi.

Aidha, Mkuu wa Mkoa amelipongeza jeshi hilo kwa kuwa walinzi imara wa raia na mali zao lakini kubwa zaidi kwa kusaidia pia katika ulinzi wa mifugo ambapo kwa kiasi kikubwa wizi wa mifugo kwa maeneo ya vijijini umepungua kutokana na uimara wa Sungusungu.
Your browser is not able to display this video.
 
Hizo haki na kanuni anazotaka sungusungu wazingatie wamejifunza wapi wakati wengi wao hata kusoma hawajui?
Hata kitabu cha katiba ya Tanzania hawajui kina rangi gani .
 
Mwambie mkuu wa mkoa upanuzi wa barabara kutoka jpm bridge busisi adi adi makaburi ya wahindi na upanuzi wa barabara toka kisesa adi nata mchakato upoje
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…