RC Mtanda: Awaahidi wafanyabiashara 802 walioondolewa ili kupisha ujenzi wa Soko Kuu la Mwanza kuwa watapewa kipaumbele katika soko

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Said Mtanda, amewaahidi wafanyabiashara 802 walioondolewa ili kupisha ujenzi wa Soko Kuu la Mwanza kuwa watapewa kipaumbele katika soko hilo ili waendelee na biashara zao, kama walivyohakikishiwa na serikali.

Mtanda ameyasema hayo alipokutana na wafanyabiashara hao, akiongeza kuwa, katika mchakato wa kuchagua wafanyabiashara watakaoshiriki katika soko hilo, wamebainika baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza wamekuwa wakilaghai wafanyabiashara na kuwatengenezea ilani feki ili kupata nafasi katika soko hilo, jambo ambalo ni kinyume na utaratibu wa serikali.

Aidha, Mtanda amesema kuwa hadi sasa amepokea malalamiko kutoka kwa wafanyabiashara ambao wameuziwa ilani feki na kwamba serikali ipo katika mpango wa kuchukua hatua kali dhidi ya wale wote waliohusika na utengenezaji wa ilani hizo feki.

Kwa upande mwingine, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Kilomoni Kibamba, amesema kuwa Soko Kuu la Mwanza lina jumla ya nafasi 1,365. Kwa sasa, kipaumbele kipo kwa wafanyabiashara 802 waliopisha ujenzi wa soko hilo. Baada ya nafasi hizo kujazwa, nafasi zilizobaki zitagawiwa kwa wafanyabiashara wengine.
 
Mara zote ndivyo huwa wanasema until it is done
 
Thubutu, imeisha hiyo,, hapo mwenye kisu kikali ndio atapewa kipaumbele
 
Back
Top Bottom