RC Mtwara: Waganga wa jadi wanaoweza kutibu mfumo wa upumuaji wajitokeze wasajiliwe

RC Mtwara: Waganga wa jadi wanaoweza kutibu mfumo wa upumuaji wajitokeze wasajiliwe

Behaviourist

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2016
Posts
39,926
Reaction score
95,626
Mkuu wa mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa, amefungua milango kwa waganga wa kienyeji na wananchi ambao wana uwezo wa kutibu maradhi yote ya mfumo wa upumuaji kufika ofisini kwake kujitambulisha ili waweze kusajiliwa kutoa huduma za matibabu kwa wagonjwa wanaosumbuliwa na maradhi hayo.

My take: Kama Taifa tumepigwa kuruhusu malimbukeni kuongoza nchi yetu.

Vyanzo: ITV, Clouds Media Twitter page

Mtwara.JPG
 
Duh ?!!!

Maisha ya watu ni muhimu hakuna kubahatisha sababu ukikosea hio sio reversible reaction

Ndio maana dawa ikitibu leo inaendelea kuchunguzwa kwa watu tofauti na kuangaliwa kwa muda kama ina side effects...

Hapa hakuna mambo ya try and error..., angeanzia kwanza kwenye kufanya majaribio kwenye panya maabara na sio binadamu..., au kama vipi ajipe corona yeye kwanza alafu afanyiwe majaribio...
 
Uzuri wa viongozi wachumia tumbo ni kwamba wanacheza mziki wa Kinje anavyotaka kulinda matumbo yao.
 
safi sana ni muda wa waganga wetu wa jadi kupiga hela
Na hizo pesa zinapigwa kwa mtaji wa watu wetu vile vile. Hii ni kama kujiibia pesa kutoka kwenye wallet yako na kuziweka mfukoni alafu unashangilia umepata faida
 
Mkuu wa mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa, amesema anawataka wale wote wenye tiba za asili za pumu, kifua, mafua maumivu ya mwili na magonjwa yote yanayohusu upumuaji

Anawataka ofisini kwake ili wajitambulishe na kuonesha namna ambavyo dawa zao zinafanyakazi kwa ili wasajiliwe ili kusaidia kwa maradhi ambayo yanayoendelea kuwataabisha watu nchini


Hii itawaa fursa kujitambulisha kwa watanzania. RC amesema uwepo wa watu wa tiba za asili ni fursa ambapo inaweza ikatatua tatizo lililopo na kuacha utegemezi wa fikra kwa dawa za wazungu
 
Isije ikawa mambo ya ramli tu, giza na nuru haviwezi changamana. Na tulishakubaliana tusali.
 
Back
Top Bottom