RC Mwanza, RPC, Brela, TRA Mwanza. Hawa Matapeli wanapatikana hapa. Wakitumia vielelezo vyenu

Mtu Asiyejulikana

JF-Expert Member
Joined
Sep 11, 2017
Posts
2,254
Reaction score
5,161
Nimeona bandiko la member mmoja akitahadhalisha kuhusiana na Ponze Scheme moja inajiita Champions Investments ltd. Inadai ipo Mwanza. Nami nimeomba Link ya kuingia kwenye group lao.

Hawa jamaa ni matapeli. Ukiangalia Hata members wao wengi ni kutoka nchi flani flani kwa mujibu wa namba zao za simu.

Lakini pia wanajichanganya admin sometime anaandika kama member kuwa naye amepokea pesa anashukuru sana. Anapost na picha yake ya bint ili kuwavutia wadada na wakaka wakware.

Nikitizama. Naona Deci hii hapa imerudi. Naiona Kalyinda hiii hapa imerudi. Naona Watanzania Hawa Hapa wanakuja Kulia kuwa wametapeliwa. Huo uwekezaji wa kuweka 50 ukapata 100 baada ya Siku tatu ni wa Sayari Gani?

ukiweka leo 10,000,000 baada ya siku tatu unapata 20,000,000. Huu uwekezaji siyo wa Sayari hii. Serikali iwasaidie wananchi. Mkuu wa Mkoa Mwanza na RPC liangalieni hili wahusika wahojiwe.

Screenshot_2022-11-29-09-57-09-453_com.whatsapp~2.jpg
 
View attachment 2430508
umeandika wanapatikana hapa lakini hujaelekeza ni wapi
 
ukiona haya yote ujue serikali inafungu.
hapa kahama wamekodi jengo la NSSF na idara zote zipo mpaka TRA.
haya mambo tumerudi kipindi cha JK
 
Huyo ni mwanaJF mwenzetu..alihaidi atafungua pyramid scheme ili kula keki ya taifa....

Tafadhari wanajukwaa tumuunge mkono ili kesho atugawie akiisha nyanyuka na kijiji...

Shukran
 
ukiona haya yote ujue serikali inafungu.
hapa kahama wamekodi jengo la NSSF na idara zote zipo mpaka TRA.
haya mambo tumerudi kipindi cha JK
Mkuu naomba kuuliza, hivi kwani huwa wanalazimisha kujiunga na hizo biashara ?

Maana kama kujiunga ni hiyari ya mtu, na watu hawataki kujifunza kwa yaliyotokea kwa DECI, Kalynda, Q-net, na mengineyo...

Basi mimi nashauri serikali iwe inachelewa kuingilia kati. Kuna watu bila kupata maumivu hawajifunzi. Unaacha wanyukwe kidogo, akili zitawakaa sawa.

Maumivu ni mwalimu mzuri sana. Mtoto akililia wembe, mpe.
 
"Siku moja mtanikumbuka, Mtasema Magufuli alisema haya" -JPM (RIP)...
Hii champion ipo tangu kipindi Cha magu nmeijua 2019 kwanza hawako mwanza hata ofisi hawana ni matapeli wajanja wajanja tu ukituma pesa wanakublock
 
Back
Top Bottom