Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Anthony Mtaka ni miongoni mwa wakazi wa Mtaa wa Lunyanywi, Halmashauri ya Mji Njombe waliojitokeza kujiandikisha kwenye Daftari la Mpiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 27, 2024.
Zoezi la kujiandikisha linazinduliwa leo Oktoba 11, 2024 na Rais Samia Suluhu Hassan huko Chamwino mkoani Dodoma na linafanyika nchi nzima.