RC Queen Sendiga: Upatikanaji wa Maji Manyara Mjini 84% na Vijijini 71%

RC Queen Sendiga: Upatikanaji wa Maji Manyara Mjini 84% na Vijijini 71%

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

RC QUEEN SENDIGA - UPATIKANAJI MAJI MANYARA MJINI 84% NA VIJIJINI 71%

"Manyara kuna hali ya hewa nzuri ambayo unaweza kulima mazao yote na Manyara ina sifa ya uwekezaji kwenye sekta zote ambazo umewahi kuzisikia. Kuna mazao ambayo hayastawi popote Tanzania isipokuwa Manyara kama ngano, shayiri, katamu utayapata hapa Manyara" - Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Mhe. Queen Sendiga

"Manyara tunalima mazao ya kipekee, mahindi meusi yanapatikana hapa Manyara na yanauzwa sana nje ya nchi. Kitunguu swaumu original kile kinatoka hapa Manyara na Mbulu" - Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Mhe. Queen Sendiga

"Mwaka 2021 upatikanaji wa maji mjini peke yake ulikuwa asilimia 68 lakini kwa sasa tunavyozungumza tuko asilimia 84 ya upatikanaji wa maji lakini vijijini mwaka 2021 upatikanaji wa maji ulikuwa asilimia 64 lakini leo tunavyozungumza upatikanaji wa maji ni asilimia 71 hivyo utaona namna gani tunaendelea kutekeleza miradi ya kimkakati" - Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Mhe. Queen Sendiga

"Jamii kubwa ya wananchi wa Manyara ni wafugaji hivyo hawakai sehemu moja, kila mtu anakaa mbali ambapo atapata nafasi kubwa ya kukaa yeye na familia yake na mifugo yake hivyo wanakaa mbalimbali lakini huwezi kuamini huko kote maji yanafika. Tumepeleka maji watu wanachota maji na wale wenye uwezo vijijini tunawahamasisha kuvuta maji majumbani kwao lakini mjini watu wanachota maji nyumbani" - Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Mhe. Queen Sendiga.
 

Attachments

  • Screenshot 2024-10-18 at 11-26-13 Clouds TV 🇹🇿 (@cloudstv) • Instagram photos and videos.png
    Screenshot 2024-10-18 at 11-26-13 Clouds TV 🇹🇿 (@cloudstv) • Instagram photos and videos.png
    803.9 KB · Views: 7
  • Screenshot 2024-10-18 at 11-26-26 Clouds TV 🇹🇿 (@cloudstv) • Instagram photos and videos.png
    Screenshot 2024-10-18 at 11-26-26 Clouds TV 🇹🇿 (@cloudstv) • Instagram photos and videos.png
    851.4 KB · Views: 6
  • Screenshot 2024-10-18 at 11-26-39 Clouds TV 🇹🇿 (@cloudstv) • Instagram photos and videos.png
    Screenshot 2024-10-18 at 11-26-39 Clouds TV 🇹🇿 (@cloudstv) • Instagram photos and videos.png
    796.2 KB · Views: 7
I am sure that the percentage figures have been picked from thin air.
Ni urongo tu.
 
Hapo vijijini amejumuisha na ya visimani itakua
 
CCM Wanapenda kujiumbua wenyewe kipindi cha Jiwe kwenye kampeni za 2020 walitaja asilimia za juu kuliko hizo. Ukifika Manyara utashangaa watu wanavyofuata maji mbali kwa kutumia Punda au kwa bodaboda.
 
Back
Top Bottom