RC Songwe: Wakurugenzi wa Halmashauri kazi zenu hazidumu milele, lipeni madeni ya Watumishi na Wazabuni

RC Songwe: Wakurugenzi wa Halmashauri kazi zenu hazidumu milele, lipeni madeni ya Watumishi na Wazabuni

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Daniel Chongolo, amewataka wakurugenzi wa halmashauri kuhakikisha wanalipa madeni ya watumishi na wazabuni bila kuchelewa.

Akizungumza katika kikao cha Kamati ya Ushauri ya Maendeleo ya Mkoa (RCC) kilichofanyika Februari 19, 2025, kwa ajili ya kupitisha bajeti ya mwaka wa fedha 2025/26, Mhe. Chongolo alieleza masikitiko yake kuhusu ucheleweshaji wa malipo hayo na kutaka maelezo ya wazi kuhusu sababu za hali hiyo.

"Lipeni madeni ya watu! Najua mlihitaji huduma hizi kwa sababu zilikuwepo kwenye bajeti, sasa hela ilienda wapi?" alihoji kwa msisitizo.

Mkuu wa Mkoa alisisitiza kuwa wazabuni hao walitoa huduma kwa nia njema, lakini wanakabiliwa na hali ngumu kifedha, ikiwemo kushindwa kulipa mikopo yao ya benki kutokana na ucheleweshaji wa malipo. Alizitaka halmashauri zote kuhakikisha wanalipa madeni hayo kwa wakati ili kuimarisha uaminifu wa watoa huduma na kuboresha utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Pia soma
~
Wazabuni na wakandarasi mnayoidai serikali mtasubiri sana, Naibu Waziri Fedha asema wanahakiki wakipata pesa watalipa

~ Tunaomba kiundwe chombo cha kusikiliza madai na madeni ya wazabuni wote wanaoidai serikali nchi nzima

~ Kada ya Afya - Halmashauri ya Kilosa hatujalipwa fedha za kujikimu, tumeambiwa hadi hali ya fedha itakapotengemaa

~ Ajira mpya kada ya afya halmashauri nyingi hatujapokea fedha za kujikimu toka November 2024
 
Back
Top Bottom