The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 896
- 1,427
Mkuu wa mkoa wa Tabora Paul Chacha ameliagiza Jeshi la Polisi wilayani Nzega kuwakamatwa Wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu waliovamia eneo la Machimbo ya dhahabu ya kikundi cha Wanawake kinachojulikana kwa jina la Mkombozi ambacho kina leseni halali ambayo imetolewa kwa ajili ya kikundi hicho cha Wanawake ambao wanajishughulisha na uchimbaji wa madini ya dhahabu.