Mkuu wa mkoa wa Tanga, Omari Mgumba ametoa kilio cha mlundikano wa wahamiaji haramu katika magereza yaliyopo katika mkoa huo mbele ya Rais Samia Suluhu Hassan hii leo.
Akizungumza mbele ya Rais Samia ambaye yupo mkoani humo kwa ziara ya siku mbili, mkuu huyo wa mkoa amesema kwamba mkoa huo una mahabusu na wafungwa takribani 2,053 ambapo kati yao, 946 wanatoka katika mataifa mengine.
Mkuu huyo wa mkoa ameongeza kuwa, kati ya hao 946, zaidi ya 830 ni wahamiaji haramu au "wasafirishwaji" ambao wameshamaliza kutumikia adhabu zao na kinachosubiriwa ni kukamilika kwa utaratibu wa kuwarudisha makwao.
Aidha, RC huyo amemuomba Rais Samia kuwahimiza viongozi wa mataifa husika kukamilisha mchakato wa kuwarudisha watu hao katika mataifa yao.