RC wa Kagera Apiga Marufuku Kuishangilia Simba

RC wa Kagera Apiga Marufuku Kuishangilia Simba

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2016
Posts
20,743
Reaction score
25,564
MKUU wa Mkoa wa Kagera, Brigedia Jenerali Michael Gaguti, amepiga marufuku wananchi wa mkoa wake kuishangilia Simba, pindi itaposhuka uwanjani leo kuvaana na Kagera Sugar.

Gaguti amefikia hatua hiyo akiwa na lengo la kuanzisha kampeni ya kuwahamasisha wananchi kuipenda timu yao na kuisapoti pindi itakapokuwa ikicheza na timu kubwa katika michezo yote ya ligi kuu msimu huu.

Kagera itakuwa katika Uwanja wa Kaitaba, kuvaana na Simba, ikiwa ni Mara ya kwanza timu hizo zinakutana msimu huu.
Akizungumzia hatua hiyo Gaguti alisema: “Umefikia wakati wa watu wa Mkoa wangu wa Kagera kuungana na kuisapoti timu yetu inapocheza na timu yoyote katika Uwanja wa Kaitaba na hatua hiyo inaanza kesho (leo) pindi Kagera Sugar itakapocheza na Simba, mkiwa huko pembeni shangilieni hizo timu zenu, ila hapa wote tunaishangilia Kagera Sugar.”

Kwa upande wa Meneja wa Simba, Patrick Rweyemamu amesisitiza wamejipanga kushinda mchezo huo na wala hawana mchecheto wowote.
 
71546898_755882761523133_1879753167931965440_n.jpg


Tujadili kwa weledi
 
Huyu mwandishi wa habari ni mchochezi.


Hebu tafuta clip ya mkuu wa mkoa wa Kagera uone.

Aliongea Tu kama mkoa wake bila chuki
 
Ila Simba mna hofu na mechi ya Leo na hii ndo itasababisha mfungwe
 
Huyo jamaa amri zake ziishie mlango wa geti la kikosi chake huko jeshini

Huku Uraini asiawaamulie watu namna ya kuishi .

Ukizoezoe toa amri unaweza amrisha Hadi kuku
 
Uzalendo kwanza,hata kama wewe ni mshabiki wa Simba/Yanga shangilia timu ya nyumbani...
 
Mleta mada, kabla ya ku-post ulijiridhisha kweli na facts? Au labda ulipata msukumo fulani kama umepigwa shoti ya umeme ukajikuta ushapost tayari!!
 
Hauwezi kuwa na akili timamu ukiwa mteuliwa katika awamu hii ukiachia ngazi ndio akili zinarudi kama umeme uliokuwa umekatika
 
Back
Top Bottom