Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Zainab Telack ametoa wito kwa wanawake wa Mkoa wa Lindi kuwa na maamuzi na ujasiri Mkubwa katika kuyafikia malengo bila kugeuka nyuma .
Mhe. Telack ametoa wito huo katika hafla iliyoandaliwa na wome's Gala 2024 yenye lengo la kuwakutanisha wanawake wakada tofauti tofauti kubadilishana uzoefu na kupata elimu mbalimbali zitakazowezesha kuwaongezea maarifa katika nyanja za kiuchumi, kijamii , kiutamaduni na kisiasa.
"Sasa akina mama ili tuweze kufika huko, kufikia malengo ambayo tunataka kuyafikia , tunachotakiwa kuwa nacho ni ujasiri mkubwa , kuwa na maamuzi ambayo hayalegilegi kwenye yale ambayo unataka kwenda kuyafikia, usikatishwe tamaa na yoyote wakati unataka kwenda mbele kama lile unalofikiria unataka kwenda nalo unauhakika utatoboa na utafika unakotaka kwenda .
Amesema hatua hiyo ya kuchukua maamuzi yanatoka na changamoto nyingi ambazo mwanamke anakutana nazo, ukilinganisha na miaka ya nyuma hasa changamoto za kiuchumi, hivyo hakuna sababu ya kutochukua maamuzi sahihi ambayo yatafanikisha kufikia ndoyo kwa usahihi bila kugeuka nyuma.
Akisisitiza hoja hiyo Mhe. Telack amewasihii wanawake lazima wazingatie kuchagua marafiki ambao wataendana na kuongeza kitu katika safari ya mafanikio kwani marafiki wananafasi ya kufanya maamuzi ya mafanikio katika maisha .
Ametumia fursa hiyo kuwahamasisha wanawake wote wa Mkoa wa Lindi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika daftari la orodha ya Mkazi ambalo litaanza Tarehe 11 hadi 20, 2024 ambapo zoezi la kuchagua viongozi/ kupiga kura litafanyika Tarehe 27, 2024 . Sambamba na zoezi hilo amewasihii na kuwasisitiza kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika maeneo yao.