Re: BRN na Wizara ya Elimu

ngumbuke

JF-Expert Member
Joined
Aug 8, 2013
Posts
495
Reaction score
527
Hivi karibuni Serikali imetangaza mpango wa Matokeo Makubwa Sasa, moja ya Wizara inayohusishwa na mpango huo ni Wizara ya Elimu.Tumeshuhudia takribani viongozi -REOs- wa mikoa kama nane wakila viapo vya kuhakikisha uwepo matokeo mazuri ya mitihani ya kuhitimu ngazi tofauti za Elimu chini ya Wizara hiyo. Mashaka niliyonayo katika ufanikishaji wa mpango huo ni
a. Je serikali imeongeza uwekezaji katika elimu? Ninavyofahamu ni kuwa mpaka hivi sasa serikali inatumia asilimia1.4 ya
pato la Taifa katika Elimu. Kwa kiwango hicho kuna matokeo mazuri?
b. Shule zetu za Sekondari zina upungufu mkubwa wa walimu hasa wa masomo ya sayansi na walimu bora wa lugha ya
Kiingereza. Je, kuna mikakati yoyote imeandaliwa kuziba hilo?
c. Sijui suala la Mitalaa kama limewekwa sawa kwani naamini Mitalaaa ya Elimu kwa shule za Msingi ni kitendawili naamini
wapo walimu ambao hawaijui au hawajawahi kabisa kuiona.
d. Hivi juzi tumeshuhudia matokeo mabovu ya Wahitimu wa Vyuo vya Ualimu ambao tunawatarajia wataingia kwenye
ajira mapema januari 2014. kwa hali hii tunatarajia BRN+ au BRN-?
Je, hao waliokuwa wakila viapo, wamekula viapo wakitambua kwamba kuna mlolongo wa changamoto kama hizo au wameburuzwa?
 
Wimbo wa kilimo kwanza umechuja. Endelea kupata sngle mpya ya brn ambayo imeshika chati.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…