Mkuu hilo suala la kuwa na "principal officer" ni sharti kwa watu wote, Agent or broker, mwezi mmoja uliopita nilikuwa nina mchakato kama wako, ila hilo suala la kuwa na huyo mtu lisikukwamishe sana, hapo unatakiwa umtafute mtu aliyesomea masuala ya insurance, mkubaliane utumie cheti chake wakati wa kupeleka usajili wako kwa ofisa wa bima. Na sio lazima awe ana bachelor, hata mwenye certificate anatosha. Na sidhani kama unahitaji kuwa na usajili wa kampuni, hayo masharti ukiyatizama yanaonekana makubwa ila yanatekelezeka bila vikwazo