pole sana mkuu, mi nadhani hili ni tatzo ambalo serikali inatakiwa kuliangalia kwa mapana yake, kwa sababu tatizo hilo la kukosekana kwa taarifa za wanafunzi wanaotakiwa kuwajibika ni chuo husika ina maana kimeshindwa kuweka kumbukumbu vizuri za wanafunzi wake.
Lakini mie nakwenda mbali kidogo kuwa hata mfumo mzima wa udahili wa mwaka huu kupitia TCU kwa wanafunzi wenye stashahada waliomaliza mwaka huu umewatenga watu hawa. Nasema umewatenga kwa sababu vyuo vingi wanafunzi wanaosoma stashahada wanamaliza mwezi huu au mwezi ujao, na mpaka matokeo yatoke inaweza kufika mwezi wa nane
sasa TCU wametoa maelekezo kuwa mwisho wa kuomba ni Juni 30 mwaka huu, sasa hawa watu ambao walitaka kuunganishia kujiunga na shahada kwa mwaka huu ina maana hawana nafasi hiyo na wanatakiwa kubaki mtaani mpaka mwakani. Hapa serikali haijatenda haki, ni bora ingeacha utaratibu wa mwaka jana wa kuomba moja kwa moja chuoni badala ya kuomba TCU ili wenye nia ya kuunganisha shahada kwa mwaka huu wapate hiyo fursa au iwaruhusu waliomaliza stashahada mwaka huu waombe mara matokeo yao yanapotoka.