Real Madrid kwenye anguko la Ottoman

Rosh Hashannah

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2017
Posts
3,415
Reaction score
2,043
REAL MADRID KWENYE ANGUKO LA OTTOMAN.

Na Haatim Abdul.

Ottoman empire ilikuwa ni himaya iliotawala sehemu kubwa ya Ulaya kuanzia mwaka 1299-1922. Yenyewe ilichofanya ni kuzivamia tawala ndogo ndogo na kuzifanya kuwa sehemu ya himaya yake. Ottoman ilitumia mbinu hiyo mpaka kuweza kuitawala Ulaya ya magharibi yote, Asia, Sehemu za Afrika ya kaskazini na magharibi kuanzia karne ya 13 mpaka ilipokuja kuangushwa na himaya ya Waroma.

Real Madrid wameweza kutawala soka la Ulaya kwa muda wa misimu 2 mfululizo na kama ambavyo Ottoman ilifanya kwenye kuziteka himaya chipukizi yenyewe Real Madrid ilizifunga timu nyingi ndogo pale La Liga isitoshe ikatanuka na kuweza kuwa bingwa wa Ulaya kwa kuwafunga mabingwa wa nchi mbalimbali lakini ni wazi kuwa utawala wao umeanza kuangushwa msimu huu.

Kwa mtazamo wangu kuna mambo makuu kama mawili ambayo yanamsumbua Zinedine Zidane msimu huu. Kwanza ni uchovu wa wachezaji ambao wamecheza kwa kiwango cha juu kwa miaka 2 mfululizo. Ni wazi kabisa kile kikosi cha ushindi ambacho kimempa mafanikio tele kimechoka. Wanasema kuwa kikosi cha ushindi huwa hakibadiliki lakini ni wazi kuwa Zidane alipaswa kuingia na mkakati mpya kuelekea msimu huu ilikujua anawezaje kuendelea kuwa ni mwenye ushindani dhidi ya wapinzani wake wakubwa huku akiona nishati (Energy) ya wachezaji hao ikianza kurudi.

Hapa ndipo Zidane alipaswa kufanya Rotation ndani ya kikosi chake lakini tatizo la Zidane mpaka sasa msimu huu ni kwamba anaishi kwa kukariri. Anachoamini mfaransa huyo ni kwamba bado anaweza kuendelea kupata matokeo kutokana na kile kile kikosi chake kilichompa mataji lukuki ndani ya hii miaka 2 iliopita jambo ambalo halionekani kuwa na uhalisia ndani yake.

Anapaswa kuwapa nafasi zaidi wakati kama kina Marco Asensio, Mateo Kovacic, Lucas Vazquez, Achraf Hakimi, Nacho, kwenye mechi nyingi za ligi lakini na vijana wengine kwenye mashindano ya makombe ambao ni wazi wamekuwa wakifanya vizuri kila wakipewa nafasi. Real Madrid imekuwa ikisifika kwa kuwa na kikosi kipana lakini Zidane haonekani kukipanua vya kutosha na badala yake anakomaa na hawa hawa kina Ronaldo, Benzema na wengineo ambao kimsingi wameshindwa kufikia matarajio ya Los Blancos msimu huu.

Lakini hata kwenye dirisha la majira ya kiangazi Zidane aliondokana na baadhi ya nyota ambao wangekuwa ni muhimu kwenye kuwapa back up wenzao waliochoka kwa sasa watu kama kina Danilo, Alvaro Morata, Pepe, James Rodriguez, Mariano Diaz n.k. Hebu vuta picha hawa wangekuwepo na hawa niliowataja hapo awali kwa pamoja ni wazi Zidane angekuwa kwenye nafasi nzuri zaidi ya kupata matokeo kuliko haya anayoyapata na hawa hawa aliowazoea ambao ni wazi wamechoka, wameshindwa kufikia matarajio na wanahitaji muda kurudisha nguvu nyingi iliopotea kwenye kujaza makabati na kumpa tabasamu raisi Florentino Perez.

Hawa alipaswa kuwafanya kama mfano wa Bima kwa maana ya kwamba anawaingiza pale ambapo timu inahitaji uzoefu wao kwenye kupata matokeo ikitokea jahazi limezama kwa vijana lakini sio wa kuendelea kuwaanzisha kila siku akitegemea kupata matokeo mazuri msimu huu.

Jingine ni hamasa. Zidane anaanzaje kuwahamasisha wachezaji wake waendelee kupigania mataji ambayo wameshashinda tayari. Ni ngumu kwa kweli. Msimu wa mwaka juzi na jana alikuwa ana kauli ya kuwaambia kwamba umuhimu wa kushinda mechi hii utakuwa moja, mbili, tatu au tujitahidi tushinde UEFA kwa msimu wa pili mfululizo na tutakuwa tumeweka majina yetu kwenye historia ya kumbukumbu ya michuano hiyo. Hapo wachezaji wanakuwa wamepata kitu cha kuwafanya waendelee kupambana lakini ana nini cha kuendelea kuwaambia na msimu huu?

Sir Alex Ferguson ametoa kitabu chake ambacho kimeeleza historia yake yote nadhani ni wakati sahihi wa Zidane kutaka kujua SAF alitumia mbinu gani kuwafanya watu kama Giggs, Scholes, Neville na wengineo kuwa na njaa ya kupambwa kila mwaka na taji ambalo walishashinda mara nyingi. Akiwa kama mwalimu chipukizi na anaetaka kuendelea kufanikiwa bila shaka akayapitie maandiko hayo na ajue namna ya kudumisha hamasa ya kushinda kwenye mioyo ya washindi.

Lakini mpaka pale atakapokubali kuanza kufanya Rotation ya kikosi chake na kuongeza hamasa ya ushindani kwenye timu basi ni wazi kuwa Barcelona au na timu nyingine pale Ulaya itamalizia kuuporomosha ufalme wao kama ilivyotokea kwa Ottoman miaka hiyo.
 
Ivi kwani Madrid na man u ni mtu na mke wake?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…