Niliona hii gemu refa alipwaya sana hasa kipindi cha kwanza kulikua na faulo nyingi sana ambazo zingine hata kadi hakutoa..
Pana ile penalt iliyochukua zaidi ya dakika tano watu wa VAR wakiangalia kama tuta kweli au laa...
Waliongeza dk 7 Diaz alipokua anajiandaa kupiga Krosi mchezaji wa Valencia alimfata Ref na kumkumbusha amalize mpira alichokifanya ni kupuliza filimbi mpira ukiwa hewani unaelekea kwa Bellingham na baada ya kufunga kwa kichwa hakusikia filimbi ya Ref ikionyesha mpira kati ndio kwanza Ref akawa anaomba mpira kwa kuashiria kuwa kamaliza mpira..
Benchi lote la Ufundi na wachezaji wa Madrid waliamka na kwenda kumfokea Ref kitendo kilichopelekea Bellingham kupewa kadi nyekundu...Mestala ni uwanja mgumu sana kwa Madrid.