Real Madrid yaweka rekodi La Liga

real G

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2013
Posts
5,227
Reaction score
5,299
Mabingwa watetezi wa La Liga klabu ya Real Madrid jana imeibuka na ushindi wa mabao 5-3, dhidi ya Real Betis na kufanikiwa kuwa klabu ya kwanza kufikisha mabao 6,000 ya kufunga kwenye ligi hiyo.


Katika mchezo huo bao la pili la Marco Asensio ambalo alifunga dakika ya 59 ndio liliifanya Real Madrid kutimiza mabao 6,000 ya kufunga kwenye ligi hiyo na kuwa timu ya kwanza kufikia idadi hiyo kubwa ya mabao.

Baada ya bao hilo la pili la Asensio lilikuja muda mfupi tu baada ya beki Sergio Ramos kufunga bao la 5,999 ambapo baadae pia Madrid waliongeza mabao mawili kupitia kwa Cristiano Ronaldo na Karim Benzema na kufanya wafikishe jumla ya mabao 6,002.

Baada ya ushindi huo wa jana Madrid imefikisha alama 45 na kuendelea kusalia nafasi ya nne kwenye msimamo wa La Liga ikiwa nyuma ya Valencia, Atletico Madrid na vinara Barcelona wenye alama 62 kileleni.

Chanzo: EATV
 
Kwa sasa madrid wamerudi kwenye ubora wao, wanaleta mkate wa kila siku kwenye mikeka ya watu, ukiwapa tu unaamka unachekelea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…