RECAP: Wanaume tuendelee kujipenda

RECAP: Wanaume tuendelee kujipenda

BabaMorgan

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2017
Posts
4,869
Reaction score
13,137
- Mwanaume usijimalize kama yule jamaa wa Mwanza, ni ujinga lakini tutaendelea kuelimishana

- Mwanaume ukijipenda...

Mwaka 2013 TV one palikuwa na kipindi kinaitwa Boys Boys kilichokuwa kinaongozwa na Mwisho Mwaipamba kipindi hicho kilibeba maudhui kuhusiana na maisha ya Mwanaume(men's lifestyle) kimsingi kilikuwa kipindi changu pendwa sababu Mabrother walikuwa wananifanya nitamani kuwa kama wao jinsi walivyokuwa wanavaa na kuongea very smart and intelligent.

Trust me hakuna furaha ya kweli kama mtu ukijipenda maana kupitia kujipenda uta attract wengi wakupende na kukuheshimu.

Kama Wanaume tumekuwa tunafeli inapokuja ishu ya kujipenda tunatumia nguvu na muda mwingi kuwapenda Wanawake na kujikuta tunasahau kujipenda mwisho wa siku wale wanawake tunaowapenda wanatuacha na kuwafuata wanaume wanaojipenda.

Mfano Mwanamke anakuomba hela ya kusuka elfu thelathini bila hiyana unatoa ila inakuwa ishu kwako kutoa elfu kumi kwenda barbershop.

Mimi nakazia tu.

1. Nenda Gym kama bajeti hairuhusu piga home workout tengeneza masculine body.

2. Viwalo saa hivi ni bei nafuu hakikisha unabadilisha nguo watu wasikukariri na nguo moja change style siku moja moja unapiga kipapaa.

3. Jadiliana na kinyozi wako juu ya style ya kunyoa inayoendana na kichwa chako ambayo itakufanya uonekane poa.

4. Accessories muhimu perfumes, cheni, saa, bracelet sio lazima viwe OG vinaweza kuwa fake vyenye muonekano wa kijanja.

5. Tembea, Mikao na kuongea kwa kujiamini sio unatembea mikono nyuma kama mfungwa onekana kama mtu mwenye mamlaka.

6. Kiatu kama ni cheusi hakikisha kweli kinangaa kama ni rangi tofauti basi kisiwe kimepauka

7. Jitahidi kula vizuri choma nyama, matunda, juice na usinywe vipombe vya buku na ikitokea hivyo basi usivinywe vikavu changanya hata na coke usije ukatengeneza sura ya kilevi.

8. Jitahidi kukaa mbali na wanawake ambao ni Totally dependent watakupa stress.

9. Angalia taarifa ya Habari, movie, comedy, series, tv shows, soma makala ili kuwa updated jinsi ulimwengu unavyoenda.

10. Jitahidi uwe na kijiwe chako kinachokupa pesa unaweza kumiliki bodaboda, taxi, daladala, au lori kutegemeana na uwezo wako.

11. Mwisho usikimbilie kuoa vuta muda atleast ukifika miaka thelathini na tano unaweza kufikiria kuvuta jiko.
 
Nakubaliana na hoja yako ya kujipenda.

Ila mtindo fulani wa u-smart kama ndio maana halisi ya kujipenda basi hapo ndio ninapoweza kutofautiana na baadhi ya watu.

Tafsiri yangu ya kuwa smart ni kuwa msafi na kuvaa nguo safi.

Hizo chains, kuinua vyuma kutengeneza msuli (attractive body) ni kujiumiza tu bure.

Zoezi ni kitu muhimu ila kufanya zoezi kwa malengo ya kuwavutia wengine naona kama ni ushamba.

Hata ukiwa home unaweza ukawa unajiweka fit unapiga pushups zako na squat fresh tu.

Sijui Perfumes, bracelet nk ni vitu ambavyo sijawahi kuvielewa kabisa.

Kwanza mimi sipendi maisha ya kuongopeana.

Yani nitumie perfume ili watu wakaribu wakinusa waseme "jamaa ni msafi ananukia fresh" wakati ile harufu sio yangu?

Hapo ni sawa uniambie "swagga ziko on" wakati umeme ni wa mgao

Au niende Gym kutengeneza six pack ili niwateke mademu?

Boshoo anasema

"Kumuamini slayqueen please usije uka test, pesa inaongea au ndio unaringia chest?"
 
Hakika love yourself, kujipenda kwangu na kujijali kunasababisha nile nyabe mpaka nizikimbie, ma zingine mpaka zinataka kulipa kwa hotel ili nizichakate, hakuna uchawi wala ndumba ni kujipenda, vaa vizuri, fanya mazoezi, kula vizuri, ishi pazuri, nukia kama lucifer...

Kila sehemu utajiamini na utaaminiwa, wale mapopoma wa kutafuta pesa na kuwapa wanawake shauri yenu, hizo pesa mnazowapa wanatumia kutulipia sisi lodge.
 
Kujipenda ni ile hali ya kujijali,kujihurumia na kijithamini...

Kuishi maisha fake uko si kujipenda....kuishi kwa ajili ya watu uko si kujipenda...

Unaishi na madeni...hufanyi kazi kutwa kupiga vibomu jamaa zako na unaishi nje ya kipato chako uko ni kujiangamiza..
 
Toka ni-date pesa sasa napendezaa na tena na enjoy! Usitafute wanawake tafuta kitu wanawake wanapenda💰😜
 
Umeongea vizuri na kama vile ulikuwa kwenye nafsi yangu vile.
 
Back
Top Bottom