Labani og
JF-Expert Member
- Sep 15, 2020
- 19,637
- 29,473
#MsasaSports
YANGA SC YAINGIA KWENYE HISTORIA
YA HIGHLIGHTS YA MECHI YAO KUWA
NDANI YA YOUTUBE YA BUNDESLIGA...
Na Godson Mbilinyi
Unapotaja Ligi Kubwa za Soka duniani huwezi kuiacha Ligi Kuu ya Ujerumani (Bundesliga) yenye klabu kubwa zinazotikisa duniani kisoka hadi kiuchumi kama Bayern Munich, Bayer Leverkusen na Borussia Dortmund sasa tuachane na hayo tuje kwenye hili la Yanga SC.
Ipo hivi wikiendi iliyopita Jumamosi ya Julai 20 Yanga ikiwa huko Afrika Kusini kwenye Pre Season tour ilipata kucheza na moja ya klabu zinazoshiriki Bundesliga ya Augsburg ambapo walipoteza kwa 2 - 1 sasa achana na matokeo mbali na mchezo mzuri walionesha Young Africans ila kimasoko imekuwa ni faida kubwa sana kuanzia kuchapishwa kwenye tovuti mbalimbali za Ulaya lakini habari nyingine ni kuwa Yanga inangia kwenye historia ya moja ya video zake kupakiwa kwenye akaunti ya YouTube ya Bundesliga.
Akaunti hiyo yenye wafuasi zaidi ya milioni 4 imepakia highlights ya mechi hiyo jambo ambalo kimasoko inawauza sana Young Africans kimataifa hivyo kuendelea kuvutia wawekezaji na hata mashabiki wapya kutoka pande mbalimbali za duniani.
#MsasaHabariSaa24