Red Bull walivyofanikiwa kuteka soko ndani ya muda mfupi kwa mbinu hii

Billy Kimber

Member
Joined
May 20, 2022
Posts
89
Reaction score
207
Red Bull ni kampuni ambayo kama umefanikiwa kuona mojawapo ya matangazo yake ya kibiashara huwa yako very interesting. Inaonekana kwenye issue ya marketing wako serious na wanachokifanya.

Mwaka 1987 kwa mara ya kwanza Red Bull waliingiza bidhaa yao nchini Austria, na walifanikiwa kuliteka soko kwa muda mfupi sana kwa kutumia mbinu hii hapa chini ya kimasoko.

Walianza kutupa makopo matupu ya kinywaji hicho kwenye mapipa ya taka na madampo nchi nzima ili kuwafanya watu waanze kukiulizia kinywaji hicho wakiamini kinatumiwa na wengi.

Na kwa hakika mbinu yao ilifanya kazi kwani watu walianza kukiulizia sana na hapo ndipo kinywaji hicho kikaanza kuuzwa na kuteka soko.

 
Biashara ni matangazo,
Sometimes tangazo linaweza kukufanya ukanunua bidhaa ambayo wala hukua unaihitaji.
 
hiyo mbinu pia tigo walitumia ,walikuwa wanamwaga simcards maeneo ya vyuo na kariakoo halafu hazijatolewa kwenye makasha,mtu anaokota anaiweka kwenye simu anatia vocha wao wanaingiza hela halafu vifurushi vyao bei rahisi

Ndo maana wanachuo wengi wakawa na simcards za tigo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…