anarchist
Member
- Apr 7, 2018
- 42
- 193
RED STAR VS PARTIZAN SIO YA KUKOSA
Ukitaja Derby hatari duniani basi hakuna derby hatari kuliko ya Red star Belgrade vs Partizan.Ubora ,utamu na uhatari wa derby hii imechagizwa na masuala ya kisiasa.Timu zote hizi mbili zimeanzishwa baada ya vita ya pili ya dunia katika nchi ya ukomunisti ya Yugoslavia wakati huo.Mnamo mwezi marchi 1945 chama cha united alliance anti fascist youth chenye mlengo wa ukomunisti wa kiharakati kutaka yugoslovia isambaratike na serbia iwe taifa huru kilianzisha timu na kuiita Red star hivyo red star ilianzishwa na Wanaharakati wakikomunisti na ikawa kama timu ya wananchi na alama yao wameandika poor na miezi michache baadae jeshi ya Yugoslavia ,Yugoslavia communist army wakati huo ukaanzisha timu yao na kuiita Partizan na klabu hii ikawa mahususi kwaajili ya watawala.Red star kama klabu ya wananchi na ya kiharakati ilikuwa inapigania utengano wa Yugoslavia lakini patizan klabu ya jeshi na watawala walikuwa wanapigania umoja na muunganiko wa Yugoslavia ukizingatia klabu ya Partizan ilipewa jina ya majeshi ya Tito yaliyoichukua Yugoslavia kwa njia ya Guerilla kutoka kwa wajerumani.Tito alikuwa mucroatia na aliiongoza Yugoslavia mpaka 1980 alipokufa,klabu ya partizan ilikuwa bega kwa bega na serikali na kupigania muungano wa Yugoslavia ambayo ilikuwa inajumuisha nchi za Slovenia,Croatia ,Bosnia ,Macedonia,Serbia na Montenegro...tofauti na Red star ilikuwa klabu ya wana harakati wa Serbia waliotaka Serbia ijitoe kwenye Yugoslavia
Deljie(Strong boys) ni jina wanaojiita mashabiki wa Red star na mabango yao huyaandika Deljie wakati Partizan wanajiita grobari sababu ya upako uliowekwa uwanjani kwao na kanisa.
Ndani ya uwanja kuna kuwa na vita kubwa kati ya wachezaji na pia kati ya mashabiki ,mechi huwa na mvuto wa pekee.wakati wa derby hii uwanja hufuka moshi mwekundu na moto huwaka kila kona huku mabaruti hupigwa na kelele za haja zikisikika na shangilia ya watukutu wa Deljie na grobari na bendera zao zikiwa na maandishi na jumbe mbali mbali zikipepea inafika wakati wachezaji hawasikii firimbi ya mwamuzi sababu ya makelele na fujo uwanjani,na mashabiki huingia na tochi kumulika uwanja ili waone sababu uwanja hutanda Giza Nene la moshi,moto mwekundu hutanda angani.
Msimu huu Red star na partizan wamekutana mara mbili kwenye ligi na mechi ya marudiano kulitokea fujo iliyosababisha watu 20 kujeruhiwa vibaya na watu wengi kushikiliwa na polisi sababu ya ugomvi na fujo na mechi ya kwanza fujo zilitokea kubwa tu.Msimu uliopita kwenye derby hii mamia ya watu walishikiliwa na polisi na wengi wakijeruhiwa na kupata vilema
Msimu wa 2015/2016 kwenye derby hii watu 50 waliumia vibaya huku polisi 20 wakijeruhiwa vibaya na watu zaidi ya 100 wakishikiliwa na polisi.
Kila msimu red star Belgrade wakicheza na partizan lazima idadi ya vifo viwepo ,majeruhi wengi wawepo na idadi kubwa ya polisi kujeruhiwa na kuumizwa vibaya ..mechi hii huwakutanisha waserbia wenyewe ,wacroatia,waBosnia na kabla ya mechi lazima kiwake,ndani ya mechi lazima kiwake na baada ya game lazima kiwake.
Grenade hurushwa kati ya mashabiki hawa ,baruti hurushiana ,Viti na ngumi hupiganwa lakini tukio ambalo halitasahaulika ni siku Red star walipocheza nyumbani kwa Partizan na mashabiki wa partizan kurusha roketi ambayo inahisiwa iliingizwa kimagendo na kiongozi wa partizan iliyompata kijana wa miaka 8 na kijana huyo kufa hapo hapo ,kwa heshima ya kijana huyo siti ile haikaliwi na mtu hadi leo kwa utukutu wa waserbia polisi wa Scotland waliwavulia kofia siku red star walipocheza na Hearts sababu fujo za mashabiki wa red star.Polisi hao walisema waliamini mashabiki wa Celtic na rangers huwa wanawapa usumbufu ila hawa wa red star ni mwisho wa matatizo,tukio lingine ni Europa league partizan wakicheza na Toulouse huku mashabiki wa Toulouse wakichomwa visu kupelekea vifo hali iliyohuzunisha kwenye tasnia ya mpira huko Italia mpaka mashabiki wa hizi timu 2 walipigwa marufuku kwenda kushangilia Europa league.
Viti jukwaani kuchomwa moto na kusababisha jukwaa kuwaka moto ni kawaida ,mashabiki kupigana huku mechi inachezwa ni kawaida ,polisi kupigana na mashabiki huku mpira unaendelea ni kawaida inafika hatua wachezaji wakati wa halftime hawaendi vyumba vya kubadilishia nguo wanabaki uwanjani kupewa maelekezo na kupumzika sababu kwenye tunnel hakupitiki moto huwaka na vita vinaendelea ni kama Mogadishu au south Sudan .
Hawa ndio red star Belgrade na partizan mpira kwao ni zaidi ya soka mpira kwao huhusisha siasa ,uhasama wa kitaifa kutoleana kejeli ,matusi kwa nchi zilizokuwa muungano wa Yugoslavia na mwisho ya yote ni vita.
Mashabiki wa Red star wanamsemo wao kufa kutetea jezi ya Red star ni ushujaa na heshima
Moyo wangu ni mdhaifu madaktari wameniambia nisiwe naenda kutizama mechi sababu nakuwa na mzuka sana.Nikiwa jukwaani nitaweza kufa lakini nitakuwepo jukwaani siku ya mechi.Kufa kwaajili ya Red star ni heshima-mzee wa miaka 62 shabiki wa red star maarufu kama mile shnuta
Deljies hawaogopi kufa wanasema walipigwa sana na mabomu ya NATO hivyo fimbo za polisi ,ngumi ,mawe za partizan ni cha mtoto hawaziogopi.Hawa deljies ambao ni mashabiki wa redstar belgrade ndio waliokuwa wanapambana na mabomu ya NATO kipindi ya vita ya yugoslavia na kikundi maarufu cha deljies ambao ni mashabiki wa redstar ndicho kilichokuwa target na majeshi ya NATO na US na war criminals wengi walikuwa viongozi wa mashabiki na mashabiki wa deljies.
Tokea 1990 Yugoslavia ilivyopasuka mechi za red star na partizan hutawaliwa na vita hakuna mechi iliisha salama bila ya polisi kuumizwa au mamia ya mashabiki kujeruhiwa na idadi kubwa ya watu kushikwa na polisi huku vifo vya mara kwa mara kutokea.
Msimu huu wamekutana mara mbili kwenye ligi na mechi zote wametoka suluhu moja moja na bila bila na vurugu kubwa zimetokea na mara nyingi derby hii huisha kwa suluhu siku timu ikishinda mbili au tatu hali inakuwa mbaya zaidi...
Siku ya tarehe 14 jumamosi jioni Red star Belgrade wanacheza play off dhidi ya partizan na mechi hii inatizamiwa vurugu kubwa kutokea na majeruhi na watu kukamatwa na hata vifo kutokea
View attachment 737220