REDIO ABOOD MOROGORO: Na methali ya Lulu vs Kanumba (R.I.P)

REDIO ABOOD MOROGORO: Na methali ya Lulu vs Kanumba (R.I.P)

TUJITEGEMEE

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2010
Posts
25,225
Reaction score
25,488
Katika hali ya kushangaza yaani isiyotegemewe hata kidogo....mtangazaji wa Redio Abood ameruhusu kusikika hewani kupitia redio hiyo methali mpya (kwangu na labda na wengine ambao walikuwa hawajawahi kuisikia). Methali hiyo imetotelewa Leo asubuhi kati ya saa 2 mpaka 3 wakati mtangazaji huyo (Mdada/Mmama) anaendesha kipindi cha Watoto.

Methali hiyo imetolewa na mtoto ambaye jina lake sikulisikia vizuri.

Methali yenyewe ilisikika hivi " UKIYATAKA YA LULU UTAKUFA KAMA KANUMBA"

Binafsi naona methali hiyo inakosa nguvu ya ustaarabu "misses moral authority" kutolewa katika jamii.

Mwanajamvi mwenzangu wewe una maoni gani ?
 
Kwenye lugha na maongezi ya mtaani (yasiyokuwa rasmi) methali kama hii siyo mbaya!! Taabu ni pale inapotumika kwenye KIPINDI kinachorushwa radioni, na kibaya zaidi kutumiwa na watoto wadogo (maana naamini kipindi chenyewe wahusika wakubwa ni watoto wa shule za msingi). Kwa kuanza kutumia misemo ya mtaani katika mambo rasmi kama kurekodiwa kwa kipindi cha radio, wanafunzi hawa usiwashangae katika mithani yao wakijibu majibu yatakayoonekana ya KIHUNI!!!
 
SURUMA Binafsi hata huko mitaani nadhani siyo vizuri methali hiyo kupata mashiko maana watoto pia wanapita huko mitaani kama suala ni kulinda makuzi mema ya watoto
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom