Kwenye lugha na maongezi ya mtaani (yasiyokuwa rasmi) methali kama hii siyo mbaya!! Taabu ni pale inapotumika kwenye KIPINDI kinachorushwa radioni, na kibaya zaidi kutumiwa na watoto wadogo (maana naamini kipindi chenyewe wahusika wakubwa ni watoto wa shule za msingi). Kwa kuanza kutumia misemo ya mtaani katika mambo rasmi kama kurekodiwa kwa kipindi cha radio, wanafunzi hawa usiwashangae katika mithani yao wakijibu majibu yatakayoonekana ya KIHUNI!!!