Lethergo
JF-Expert Member
- Aug 7, 2023
- 6,534
- 11,421
Salamu Wakuu.
Niende moja kwa moja bila kuwachosha wala kuwapotezea muda.
Hili suala la Redio na Tv na kamari sasa ishakua kero yaani unakuta kipindi cha Redio au kipindi cha Televisheni Mtangazaji mwanzo mpaka mwisho hakuna anachotangaza chochote kipindi kimepewa Jina jingine ila kinachofanyika kwenye kipindi ni kingine, kwanini kipindi kisiitwe tu kamari ili watu waelewe kwamba hapa nimefungulia Redio nasikiliza kipindi cha kamari au nimefungulia Televisheni naangalia kamari? Kwanini isiwe hivyo?
Zamani kulikua na 'Jackpot Bingo' ilikua haimisiwi hivi ilikua na muda maalum na mtu ukiangalia unajua kabisa muda huu naangalia kamari.
Mamlaka zinazohusika basi angalieni namna ya kuweka hili jambo sawa, sasa tumechoka na hizi kamari yaani kipindi unasikiliza mwanzo mpaka mwisho ni kamari kamari kamari ooh huyu ameshinda laki 2 weka 1000 ushinde laki 2 ooh huyu ameshinda laki 5 weka 1000 ushinde laki 5 ooh huyu ameshinda million weka 1000 ushinde million, jamani tumechoka sio wote wacheza kamari.
Mamlaka zinazohusika Bodi ya Michezo ya kubahatisha na TCRA na wengineo ziwaambie wenye kuhusika na redio TV na wamiliki pamoja waendesha vipindi, vipindi vya kamari ni bora vibadirishwe majina na viwekewe muda wake maalum ili mtu ajue kabisa hapa ninasikiliza hiki kipindi nasikiliza kamari tu sio kipindi kinapewa jina jingine ila mwanzo mwisho mtu unasikiliza kamari tupu.