Ambiente Guru
JF-Expert Member
- May 21, 2012
- 2,605
- 1,085
Nimesikia redio za hapa nchini (Mfano za Rev. Dk G. Rwakatare na Rev. Mtume Ephata) kutumia neno "Kumwambukiza" mtu uwezo au kipawa cha kufanya miujiza au upako. Je ni kiswahili sanifu?. Neno "kuambukiza" linatumika kwenye mambo chanya au hasi? TV na Redio watangazaji lafudhi zao zinapotosha kiswahili (ITV, Ch 10, ) mfano kusema; Malelia au marelia badala ya Malaria. Badala ya li wanaweka ri. Wanaweka msingi mbovu kwa watoto na wanaweza kuwafelisha mitihani.