DOKEZO Redio Tanzania - TBC ni majanga mikoa ya Rukwa na Katavi

DOKEZO Redio Tanzania - TBC ni majanga mikoa ya Rukwa na Katavi

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Izia maji

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2021
Posts
2,997
Reaction score
5,385
Sifahamu kama serikali ya Samia inathamini wananchi wa mikoa hii miwili katika suala la kupata habari kutoka chombo cha umma ambacho kodi zao zinachangia kukiendesha.

Usikivu wa TBC ni wa hovyo kupita maelezo na inaelekea na viongozi wa mikoa hii ama hawajali au wamekata tamaa. Nao viongozi wa TBC wamelala usingizi wa pono kama vile kila kitu kiko sawa!

Ni aibu kwa serikali hii ambayo kila kukicha ni tambo za kujisifia mafanikio yake! Sasa kama kuimarisha usikivu wa redio tu umeshindikana wananchi wa mikoa hii waiamini kwa lipi?

Wana Rukwa na Katavi wana haki ya kusikiliza redio wanayoilipia kodi na si kwamba wanaomba hisani!
 
Ni hujuma na ufisadi wa kutisha , huwa sijui kwa nini Africa hata huduma ya posta imekufa🤔
 
Achaneni na TBC fuatilieni Wasafi fm mpate taarifa za uhakika na kwa ubora wa hali ya juu
 
Yeah najua , ila kiujumla ningependa kujua🤔
Umeshajiupiza why meadia za private zinakimbiza kuliko radio tz na tbc?

Private sector wanatembea na performance zaidi , wakiwa bora wanapata faida. While gov funded hawajapi sababu hata wasipo perform mshahara utaingia tu. Hamna hasara pia
 
Hiyo inaonyesha Africa ni sehemu ya kipumbavu sana kufanya maisha seriously
 
Yeah najua , ila kiujumla ningependa kujua🤔
Moja ya sababu ya posta kufa Tanzania ni uzembe! Parcel kutoka Dodoma hadi Sumbawanga inachukua siku 7 wakati kwa mabasi binafsi ni siku mbili, yaani ikitumwa leo kesho inapokelewa.

Kwa kutumia busara za kawaida hakuna mtu ataenda posta na hasa ukizingatia urasimu utakaokutana nao!
 
Africa sijui tupoje
 
Back
Top Bottom