Reflections

Reflections

Shayu

Platinum Member
Joined
May 24, 2011
Posts
608
Reaction score
1,655
Kila wakati sisi binadamu ni muhimu kupata nafasi ya kufanya reflection. Tafakari ya kina kuhusu maisha yetu, kuhusu tabia zetu, kuhusu uwepo wetu duniani. Kuhusu mahusiano yetu. Ukuaji wa binadamu sio mwili tu bali pia na akili. Lakini bila kufanya reflection ukuaji wetu wa kiakili unakuwa mdogo. Ni muhimu kutafuta sehemu. Kutafuta chumba sehemu ambayo ni tulivu. Chumba ambacho kitakuwa maalumu kwa kufanyia reflection. Bila kufanya reflection au meditation hatutaweza kuungana na spirit ambayo ina hazina ya maarifa yaliyojificha.

Tunapotafakari kwa kina ( reflection au hata meditation) tunaungana na spirit ambayo ninaweza kusema ni mungu. Huko tunapata majawabu yetu yote kuhusu maisha. Tusipuuzie kutafuta muda na kukaa peke yetu kufanya reflection. Watu hutoka hata kwenda mbali porini kufanya reflection. Bila kufanya reflection huwezi kumjua mungu wako.

Mungu wako yuko ndani yako. Ni spirit ambayo iko ndani yako. when you converse with him anakueleza kipi cha kufanya na kipi cha kutokufanya. Kwahiyo mungu yuko ndani ya kila mtu. Katika biblia wanasema tumeumbwa kwa mfano wake ni hiyo spirit ambayo iko ndani yako. Ambayo ukitenda maovu inakusuta. ''We are the temples of God'' mungu anaishi ndani yetu.

When we pray and when we reflect we invoke him. Lakini pia reflection au hata meditation inasaidia ku control mawazo yetu. Mawazo yetu; yaani jinsi tunavyofikiri ndio chanzo cha furaha au huzuni ya mtu katika maisha. Kwahiyo siri ya furaha ni kudhibiti jinsi tunavyofikiri kwa ku control mawazo yetu. Hii ni ngumu inahitaji nguvu za kiakili (concentration kubwa ) kudhibiti na kuongoza mawazo katika mkondo unaofaa. Inahitaji combination ya faith and concentration.

Kwahiyo mlolongo wa mawazo ambayo ni hasi na mashaka hufanya maisha ya binadamu kuwa yasiyo na furaha. Kwahiyo mind zetu mara nyingi zinakuwa passive na zinapokuwa passive zinaruhusu mlolongo wa mawazo ambayo ni negative. Reflection inaongeza thoughtfulness.

Kwahiyo jinsi tunavyofikiri ni chem chem ya uhai. ''We must guide how we think'' Kwahiyo we must pray to God everyday atupe nguvu ya kuweza kudhibiti mawazo yetu. Struggles katika maisha lazima zitakuja kukupima kiwango cha imani yako kufanikiwa au kushindwa katika struggles zako kutategemea sana na kiwango cha imani yako. Binadamu hawezi kukua pasipo struggle, hutufanya tuwe imara. Mawazo hasi pia hutufanya tujihisi hatuwezi hivyo ku retreat.

Kwahiyo jinsi tunavyofikiri na imani yetu ndivyo vinavyotuongoza. Mimi ni miongoni mwa watu ambao wanahangaika kila siku na imani yangu pamoja na fikra zangu. Mashaka hunitawala kama binadamu wengine, kila siku nahangaika ili nipate imani na kuwa na mawazo yasiyotetereka.

Na maono lakini maono hayo sitoyafikia kama nitakuwa na mashaka katika kila ninachokiamini.Kwahiyo kila siku nawajibika kumuomba mungu aongeze nguvu zangu ili kile ninachokiamini, maono yawe kitu dhahiri machoni mwa watu. Nafanya reflection mara kwa mara. Ni muhimu kwa kila mtu. socrates aliwahi kusema ''unexamine life is not worth living'' Akimaanisha tunapaswa kufanya reflection ya maisha yetu mara kwa mara. Kwahiyo tafuta kiti tafuta sehemu tulivu chumbani fanya reflection. Ni muhimu sana. Think Think.
 
Back
Top Bottom