Gandhi
New Member
- Jul 25, 2022
- 3
- 1
Ni ukweli uliowazi kwamba jina Reginald Mengi sio jina geni Hapa, kila mmoja alimjua au kumfahamu kwa namna yake, hata kama hukuwahi kuwa karibu naye, kama mimi ninayeandika haya, lakini haikudhuia kumfahamu kama sio kwenye Utajiri wake, bhasi shughuli zake na haswa akiwa Nguli katika Tasinia ya Vyombo vya habari.
Wakati nilipokuwa mdogo nilikuwa nikitizama ITV lazima nimuone na alipokuwa akihojiwa alikuwa anachukuliwa mda mwingi kiasi ambacho nilikuwa nachukia nikawa nawauliza Baba mbona huyu anahojiwa sana, baba akaniambia huyo ndo mwenye Channel, na ukizingatia Mengi alikuwa anaongea taratibu kwa sauti ya chini (upole).
Msishangae ni akili ya utoto kwani baba yangu alikuwa ananilazimisha kutizama Taarifa ya Habari nikiwa mdogo kitendo ambacho tulikuwa tunachukia kama watoto unakuta anatoa Tamthilia ya Day of Live kipindi hicho, Hivyo Mengi nilianza kumfahamu kwa kumuona kwenye Television ya Panasonic mwaka 1997.
Na hata mwangaza wangu wa kumfahamu Mengi ulishia Hapo lakini mwaka mmoja nakenda baada ya kifo chake may 2 mwaka 2019 nimebahatika kusoma kitabu chake alichokiacha cha “I Can, I Must, I will. Alichoandika kwa lugha ya kimagharibi japo alikuwa na ndoto ya kuweka katika Lugha ya kiswahili, hili kiweze kusomwa na watu wengi zaidi.
Msukumo wa pili wa kusimulia yaliyomuhusu Mengi, ni ukweli uliowazi yawezekana tangu Tanganyika na mpaka Tanzania hatujawahi kubahatika kupata Mtu mweusi mwenye Ukwasi kufikia au kumzidi Mengi.
Yasemekana Utajiri wake ulifikia USD 560 million ambao kwa hela ya kwetu kama Trilion 1.5 kwenda 2 hivi.
Hivyo kwenye Orodha ya Mabilionea Nchini alikuwa Mswahili pekee anayechomeza mbele ya watanzania wenye jamii ya kiasia, tena akingia nafasi ya nne au ya tano nyakati zote. Sio swala haba na ningependa nieleweke kwamba nakala hii sio ya kibaguzi kwa matajiri wengine lahasha ! kwani hata Magazeti makubwa Duniani yalishawahi kutoa Orodha ya Mabilionea weusi (Black Bilionea) ambapo Dangote akaendelea kuwa kinara
Msukumo wa tatu kuandika kuhusu yeye, nikutaka kuonyesha amewezaje kujijengea mafanikio hayo yote na haswa ni kitambua Utajiri hakui kama Uyoga Tu wiki tatu unaota, hivyo nilijua Mengi amepita katika vipindi mbalimbali vya awamu ya kiserikali kuanzia nyakati za Mwalimu wakati Taifa likiwa Changa kabisa hii ilinichochea mno, kwani binafsi naamini kizazi cha dhahabu (gold generation ) Tanzania ni kizazi cha akina Mwalimu yaani 1920,40s na 60s .
Email :- mathewambajo@gmail.com

Upvote
0