Reginald Mengi '1m price for a nice tweet'

Status
Not open for further replies.

Mlachake

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2009
Posts
4,437
Reaction score
4,618
[h=3]Upo kwenye Twitter? Kama haupo fanya haraka

ujiunge sababu kuna ulaji huko!! Mwenyekiti mtendaji wa makampuni ya
IPP, Reginald Mengi amesema kuanzia mwezi huu, atakuwa akitoa shilingi milioni 1 kwa kila tweet itakayomfurashia.

Not to fast
though…… Sio tweet zile za ‘I’m having fun being single, #TeamSingle, tupa
kuleee!

Mengi anataka ulikune
jicho lake kwa tweet yenye akili ambayo inaweza kuchangia kwa namna moja ama
nyingine kupunguza umaskini uliokithiri nchini.

“Umaskini umekuwa sugu. Kwa mwaka 1 anzia Mei ntatoa sh 1m
kila mwezi kwa tweet nitakayochagua kuwa bora kushinda vita na umaskini,”
ametweet leo.


Ameongeza kuwa Tweet hiyo iende kwake, yaani mtu
akiandika tweet afanye kummention ili aione.
[/h]
 
Nitajipatia hiyo milioni aisee..
 
Akumbuke kuwalipa vizuri wafanya kazi wake ili hiyo pesa ikapunguze umasikini kwenye familia zao na siyo kuwaacha wanapiga mihayo tu. Hili ni wazo la kuanzia.

La pili hiyo pesa aanzishe mkakati wa kilimo cha mboga au mazao yenye soko la uhakika na awape tu vijana watakaokubali kuhama mjini na kwenda kushiriki kwenye hicho kilimo.

Desa hilo nenda mka mtweet!
 

sorry dude this is too long for tweeting aisee..
 


Ha ha ha ha ha ha yaani uwachukue wale jamaa pale ubungo waache kupiga debe wakalime Mboga,

Wazo lako zuri sana kaka, Kilimo kinalipa sana sijui ni kwanini watu wanazunguka na vibahasha vya kaki kule posta na tai wakati jua linachoma mwanzo mwisho.

Hebu ngoja nim tweet huyu mzee
 
Afadhali watu wengi wameanza kujiunga MKURABITA!!!!!!!!!!! Kweli Umasikini umekuwa sugu!

Max na Mike muwe mnatoa hata 10,000/= kwa kila thread itakayosaidia kupunguza umasikini!!!!!!!!!!! Join the rhythm guys. ITS TIME FOR CHANGE!!!!!!!!!!!

Ngoja nikajiung twitter! Nikishinda tweets 10 tayari zile M 10 za kuzungusha afu watu wanasema Tz hamna fursa? Fursa hiyo!
 
Upo kwenye Twitter? Kama haupo fanya haraka ujiunge sababu kuna ulaji huko!! Mwenyekiti mtendaji wa makampuni ya IPP, Reginald Mengi amesema kuanzia mwezi huu, atakuwa akitoa shilingi milioni 1 kwa kila tweet itakayomfurasha

Mengi anataka umkune mtima wake kwa tweet yenye akili ambayo inaweza kuchangia kwa namna moja ama nyingine kupunguza umaskini uliokithiri nchini.
“Umaskini umekuwa sugu. Kwa mwaka1 kuanzia Mei nitatoa sh1m kila mwezi kwa tweet nitakayochagua kuwa bora kushinda vita dhidi ya umaskini,” ametweet leo.
Ameongeza kuwa Tweet hiyo iende kwake, yaani mtu akiandika tweet afanye kummention ili aione. Hiyo ndiyo habari ya mjini....kazi kwenu wazee wa Twitaaaaa..........
 
Vigezo na masharti kuzingatiwa....subirini muone kama mtapata!!
 
Akitaka kusaidia kuondoa umaskini awahamasishe matajiri wenzie wasikwepe kodi bali wailipe serikali kodi stahiki.
 

Hiyo sasa ni ya kwako mkuu!
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…