Rehema Mwakangale hayupo nasi

RIP Rehema.

Namkumbuka Rehema hususani kipindi kile wakati anaanza kusoma taarifa ya habari akiwa na Iddi Ligongo... Alianza kwa kusuasua lakini baadaye akawa mtangazaji mahiri wa habari ya TV wa ITV.

Taa na nuru iliyokuwa inang'aa imezimika ghafla.

Tutakukumbuka daima Rehema!!!
 
Inasikitisha lakini ndio njia yetu sote Kinachonihudhunisha ni ucheshi na utaratibu wa Marehemu Rehema Hapakuwa na Presenter aliekuwa mfano wake hakuwa na majivuno Ni Mtaratibu Mkimya Na Alikuwa na Busara Mwenyezi Mungu ailaze Pema Peponi Roho ya Marehemu -Aamin
 
Poleni wafiwa.
Ni safari ya wote ila kutangulia ndiko kugumu!
Pumzika kwa amani rehema.
 
duh! hakuna atakayeishi milele, sote tu wapitaji hapa duniani.
poleni wafiwa, itv na wanahabari wote.
 
Dah RIP Rehema, poleni sana Ndugu na marafiki
 
Poleni wafiwa, mwakanale ni msiba wetu sote. Pia tujue kwamba kifo kimeumbwa kama tulivyoumbwa sisi. Hivyo ili kiendelee kuishi lazima binaadamu tuendelee kufa. Hii maana yake huu ndio mfumo wa maisha
 
Jamani Rehema! Its too sad.

Pumuzika kwa amani dada, nasi tuko nyuma yako
 
Bwana alitoa, na Bwana ametwaa, jina la Bwana na libarikiwe....
 

Tunaweza pata kidogo historia fupi ya marehemu?
Jamani mwenye data p'se.
Tupo pamoja ndugu,rafiki,wapenzi wa ITV na maadui katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.

Ni kweli kabisa.

Wafiwa poleni sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…