Kwani nani amesema haufi? Hapa mleta mada anamaanisha baada ya kifo, kwamba kuna uwezekano mtu akazaliwa kwenye mwili mwingineAliyetueleza ametuumba kwa utaratibu huu na huu, na sayansi imethibitisha ndio yeye ametueleza tukifa tunaenda wapi, na uhalisia ni shahidi mzuri, umeona mtu amekwepa kifo?! hata uwe Buddha wa nyota 70 siku ikifika unaenda na maji kirahisi sana, so na wewe ukiuza simu punguza kujipa matumaini jiandae na mauti yako.
Unauhakika au unaishi katika kile ulichokaririshwa na maandiko ya waarabu.nzalendo
Ukishaondoka duniani haurudi tena mkuu utabakia kwenye kizuizi kaburini mpaka siku ya kufufuliwa kwaajili ya kulipwa wema kwa wema na ubaya kwa ubaya, najua ni mtu mzima sasa, punguza haya matumaini na ujiandae na mauti yako.
Unaweza ukafa ukazaliwa kama Al Shabab, halafu na wewe unaanza kuua watu kisa imani zao 😁Kama ni hivyo ni poa tu nikifa nikazaliwa tena kwa Trump itakuwa unyama tu.
Ndugu usiniwazie mabaya basi, bora uniombee nikawe hata mjukuu wa Iron Musk na siyo hayo majambalika.Unaweza ukafa ukazaliwa kama Al Shabab, halafu na wewe unaanza kuua watu kisa imani zao
Ukiondoka unaenda wapi au na wewe haujui?nzalendo
Ukishaondoka duniani haurudi tena mkuu utabakia kwenye kizuizi kaburini mpaka siku ya kufufuliwa kwaajili ya kulipwa wema kwa wema na ubaya kwa ubaya, najua ni mtu mzima sasa, punguza haya matumaini na ujiandae na mauti yako.
Ukifa unazaliwa nch nyingineNaam hili jambo nilikuwa nalichukulia poa...lakini baada ya kuamua kufuatilia kidogo naanza kupata uthibitisho pasi kuwa na shaka juu ya mzunguko wa maisha ya viumbe sisi bin adamu.
Kwa kifupi sana tafiti ni nyingi lakini......nilipata kuishi nyanda za juu kusini mwa Tanzania nikiwa kijana mdogo miaka mingi sana iliyopita.
Nilikuwa nina rafiki yangu Mbulushi...rafiki yangu huyu kwa bahati mbaya alifariki.
Siku ya siku sina hili wala lile nikiwa katika nchi ya mbali sana nikakutana na kijana mmoja amefanana na yule rafiki yangu kwa zaidi ya asilimia 90%...nikabaki namshangaa...kitu cha ajabu na yeye kama alikuwa ananishangaa...nikamuuliza ulishawahi kuishi.
Tanzania...akasema hapana hata Neno Tanzania ndio leo analisikia.
Ajabu zaidi anasisitiza kwamba ananifahamu lakini hakumbuki ni wapi tulisha kuwahi kuonana
Mahali ambapo nilipata mshituko niliona alama katika mkono wake wa kulia sawasawa na yule rafiki yangu,,,(alama hii naikumbuka kwa sababu alianguka na baiskeli akachanika na kushonwa katika hospitali ya Aga khan)....sasa huyu jamaa anasema hiyo alama amezaliwa nayo hivyohivyo.
Nikijaribu kumuuliza yeye asili yake ni wapi anasema ni Afganistan na hana ndugu wala jamaa Afrika.
Kwa kifupi sana 1.Sauti yake 2.Ongea yake 3.Namna anavyotembea ni yule marehemu kabisa kabisa.
Yule Marehemu leo angekuwa na miaka kama 70 hivi na huyu niliyekutana nae yuko kwenye miaka ya 30 katikati.
Kwanza thibitisha roho ipo.Roho ya binadamu ina mzunguko mrefu sana wa kuishi ulimwenguni, ila bado najiuliza kuhusu viumbe wengine kama mapaka, simba na madog.
Dhana ya Ukifa hauendi popote ni uongo kwasababu hakuta kuwa na 'wewe' wa kwenda popote. Kama ambavyo hakukuwa na 'wewe' kabla hujazaliwa..ndivo itakavokuwa utakapokufa.Hata mimi nahisi hatufi mazima
Lakini kuna dhana ambayo naona ipo sahihi zaidi. Nayo ni kwamba ukifa ndio unapotea mazima, haurudi tena duniani na ndio inakuwa imeisha hiyo
Hii naiamini kwa asilimia nyingi zaidi, japo kuna muda nikiwaza hata hiyo ya kwamba ukifa unazaliwa tena inamake sense kuliko hizi habari za kwenda motoni na peponi