REKODI-Mgeni ambae huonekana mara moja duniani.

Idd Ninga

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2012
Posts
5,497
Reaction score
4,775
MGENI WA MWAKA.

1)Tumesubiri kwa hamu,kukwona mgeni mwema
Nyingine hii yetu zamu,kufikwa tu wazima
Tulikuwa to fahamu,tungekwona ewe mwema
Mgeni mwema wa mwaka,karibu kwengu nyumbani.


2)Muda umeshawadia,kufanya toba kwa sana
Dhammbi tulokusudia,na za siri kuachana
Kabla tujaangamia,na gharika kukumnana
Mgeni mwema wa mwaka,karibu kwengu nyumbani.



3)Maovu kuyachukia,mema kuhamrishana
Nasaha kujiusia,maovu kukatazana
Na madhambia kujutia,kwa kheri kukusanyana
Mgeni mwema wa mwaka,karibu kwengu nyumbani.



4)Kwa mwaka ni Mara moja,mgeni tunaonana
Shahari hatotungoja,ni kesho tutaachana
Kwa Mara moja ye huja,na kisha tunatengana
Mgeni mwema wa mwaka,karibu kwangu nyumbani

Shairi-MGENI WA MWAKA
Mtunzi-Idd Ninga,Arusha
iddyallyninga@gmail.com
+255624010160.
 
labda mnichangie kwanza.
maana Arusha hadi Iringa ni mbali sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…