Rekodi muhimu za Simba na Yanga tangu 1938

hiram

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2013
Posts
266
Reaction score
393
Kumbukumbu muhimu Kuelekea Tarehe 12
1. Yanga inaongoza kwa kumfunga Simba mara nyingi wakati Simba ndiyo timu ya kwanza kuvaa viatu hii ilikuwa1949 ilipocheza na kombaini ya jeshi la majini Navy ya Afrika Kusini.

2. Yanga ndiyo iliyochukua ubingwa mara nyingi zaidi (27) kuliko timu yoyote wakati Simba ndiyo timu ya kwanza kuvaa jezi hii ilikuwa 1938 ilipocheza na kombaini ya mabaharia wa meli zilizotia nanga kwenye bandari ya Dar es salaam.

3. Yanga ndiyo timu ya kwanza kutinga robo fainali ya CAF champions league mwaka 1969 (dhidi ya Nkana Red devils) wakati simba ndiyo timu ya kwanza kupanda ndege mwaka 1963 walienda Ethiopia kwa mwaliko wa Rais wa nchi hiyo.

4.Yanga ndiyo inaongoza kwa idadi ya magoli yaliyofungwa kwenye mechi za Simba na Yanga wakati Simba ndiyo timu ya kwanza kuvaa suti hiyo ilikuwa ni mwaka 1974 ilipokwenda Poland

Kutoka kwa mwalimu wa Takwimu
 
Ndio rekodi hz tako moja huwa anazitumia kuwalaghai hawa mbumbumbu
 
Kumbukumbu muhimu nyingine ni Simba ndio timu iliyopata magoli mengi zaidi dhidi ya Yanga. 6-0, 5-0, 5-0.

Vv
 
Kwa hyo ile ya Simba kukimbia mechi baada ya dakika 45 za kipindi cha kwanza kutokana na mchezo kuwawia mgumu na hatari sana kwao ni ndogo?
 
Kumbukumbu muhimu nyingine ni Simba ndio timu iliyopata magoli mengi zaidi dhidi ya Yanga. 6-0, 5-0, 5-0.

Vv
Kuweka kumbukumbu sawa Yanga ndie wa kwanza kumfunga Simba 5-0 1968 na mwaka uliofuata Simba gari lao liliishia chuo cha duce pale hawakuingia uwanjani kuogopa 5 zingine mwaka 2012 Simba akalipa kipigo cha 5-0 Kwa hivyo deni ambalo tunadaiwa wananchi ni 6-0 hizo 5-0 bila zako mara mbili naomba nikumbushe hiyo nyengine ilikuwa mwaka gani? Tatzo mashabiki wengi wa simba mmeanza fatilia mpira uongozi wa rage na hanspope kipindi watoto wa mjini tunabebwa na baba zetu kwenda green stand (shamba la bibi) kuzicheki Simba na Yanga wengi wenu mlikuwa butimba huko ndanindani!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…