Rekodi ya matukio kadhaa yaliyotokea Qatar kwenye kombe la dunia hadi sasa

marcoveratti

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2017
Posts
1,019
Reaction score
1,824
Mashindano Ya kombe la Dunia Yakiwa Yanaendea Kuna Baadhi Ya matukio na Rekodi kadhaa ziliwekwa na Timu na wachezaji Binafsi.Hizi ni Baadhi Ya Rekodi katika mashindano.

[emoji429]Qatar imekuwa timu Ya kwanza mwenyeji kupoteza mechi Ya Ufunguzi, Timu Ya kwanza Kuondolewa katika mashindano baada Ya michezo 2, Timu Ya kwanza mwenyeji kuondoka na Alama 0 na kushika mkia katika Group.
Gracias Qatar[emoji110] ,Qatar Wame set standard Namna gani Ya kuandaa Mashindano

[emoji429] Atiba Hutchinson ameweka rekodi Ya kuwa mchezaji mkubwa zaidi kushiriki Kombe la Dunia nchini Qatar akiwa na miaka 39 ni mkubwa kwa zaidi Ya Siku 100 kumzidi Dani Alves wa Brazil.

[emoji429]Gavi ndio mchezaji mdogo kufunga katika mashindano Ya kombe la Dunia Huko Qatar, Akiwa na miaka 18 Tu na mchezaji mdogo kucheza Mashindano hadi sasa.

[emoji429]Mechi iliyowakutanisha Korea kusini dhidi Ya Uruguay ilitamatika bila ya kupigwa shuti lolote lililolenga lango, Ni Rekodi na mara Ya kwanza katika historia Ya Kombe la Dunia kwa Karne Hii.

[emoji429]Enner Valencia Amekuwa mchezaji wa kwanza kufunga goli la Kwanza la Kombe la Dunia nchini Qatar . Amekuwa mchezaji wa kwanza kushinda Tuzo ya mchezaji bora wa mechi .

[emoji429]Cristiano Ronaldo ameweka Rekodi Ya kuwa mchezaji wa kwanza Kufunga katika Kila mashindano Ya Kombe la Dunia aliyocheza ,ameshirikia fainali kombe la Dunia mara Tano
2006, 2010,2014, 2018 na 2022.

[emoji429]Robert Lewandoski amefunga goli la kwanza katika mashindano Ya kombe la Dunia (alikuwa hajawahi Funga katika Kombe la Dunia).

[emoji429]Ushindi mkubwa kwa Timu katika mashindano ni Waliopata Hispania dhidi Ya Costa Rica wa 7-0 Na Senegal wamekuwa Timu Ya kwanza kutoka bara la Afrika kufuzu hatua inayofuata
Bravo [emoji110].

NB:MATUKIO GANI NA REKODI NYINGINE UNAYO YAKUMBUKA YALIYO TOKEA QATAR MPAKA SASA

Credit Dezo Maesto Twitter

.View attachment 2431887
 
Kuna tunaongalia nani kafungwa na nani kafunga na kuna mnaoangalia mchezo mzima kuanzia kikosi,uchezaji wa mmoja mmoja na kila kitu kinachohusu mchezo. Hongereni sana ila na sisi ni wa muhimu tupo kama wachangia chochote kuna mambo hapo ndo nayajua leo mfano hyo ya korea kusini na uruguay 😀 😀 😀 😀
 

Rekodi ya mwanasoka mdogo zaidi kucheza kombe la dunia na kufunga goli iliwekwa na Pele mnamo 1958 na kuisaidia Brazil kubeba kombe ilo uko Sweden , Pele alicheza kombe la dunia kwa mara ya kwanza 1958 na kuweza kufunga goli akiwa na umri mdogo wa miaka 17 tu, Na rekodi iyo haijawai kufunjwa mpaka leo hii .
 
Unapotaja mchezaji ni vyema ukataja na taifa analochezea ungeeleweka zaidi
 
Umetaja wachezaji lakini timu zao hujazitaja.
Msomaji wa komenti asiyewaelewa wachezaji hao, je hatatambua vipi nchi wanazoziwakilisha?
 

At 37 years and 247 days old, Steve Mandanda become the oldest player ever to appear for the French national team, surpassing Bernard Lama from September 2000 v England (37 years and 148 days).

 

Nimechangia humu hii thread lakini cha ajabu nimeenda twitter nimekuta andiko kama ili yaani Copy and paste, Nmeshindwa kuelewa aliepost uku na twitter ni mtu mmoja au ni nani amecopy kwa mwenzake? Tufike maala wa Tanzania tujue kutumia akili zetu vizuri lasivyo tutoe Respect kwa waanzilishi wa mawazo.
 
Time angalia is nani kaanza kupost utajua nani kakopi nani kaandika
 
Ronaldo kashiriki fainali mara tano zipi...??
Robo au nusu.
Au fainali kamili..!?
Maana sijakuelewa hapo
 
Time angalia is nani kaanza kupost utajua nani kakopi nani kaandika

Nikiangalia muda basi yaonesha uko twitter ilikuwa ya kwanza kabla yako kupost uku JF, kwa kigezo iko basi wewe ndio umecopy maaana haijabadirishwa ata neno moja aseeh. Ila sio tatizo japo ulitakiwa kuonesha uungwana wa kutoa credit kwa alieandika.
 
Hili la Senegal pengine labda umetumia tungo tata. Unamaanisha nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…