Kasie
Platinum Member
- Dec 29, 2013
- 22,379
- 41,294
Hello Ladies and Gentlemen at MMU, it has been long time haven't had my pen and paper but today I have a piece to share and discuss if you won't bother neither mind....!!
The matter on the table is personal and it depends with culture and how one was raised...
NB allow me to mix language so as open wide discuss and receive different views 😊.
Kichwa cha mada ni mahusiano kati ya mzazi na watoto ukilinganisha mahusiano ya mzazi na wanyama kama mbwa paka na jamii ya wanyama wafugwao.
Dunia inaenda kasi sana, imefikia kipindi mtu anaona kuwa na mtoto wa kumzaa au wa kumlea ni kadhia na historia inatupa taswira.
Kuna wazazi walifanikiwa kupata watoto wa kuwazaa kuwalea watoto na mwisho wa siku watoto wakageuka kuwa mwiba kwa wazazi hao, kama ushawahi sikia jina la Mzee Kuzaa Si Kupata....
Kuna waliofikia umri wa kuwa na watoto ila sababu ya ugumu wa maisha wakaona bora wasizae ila bora wawe na mnyama wa kufugwa (paka/mbwa) walau awaondolee upweke.
Binafsi wakati nakua wazazi wangu walipenda mbwa, ila walikuwa wale mbwa wa kukaa banda la nje, marufuku kuingia ndani, ila tukiwa watoto tulicheza na mbwa na hata mtaani tulitoka nao na ilikuwa ubabe flani hivi hakuna wa kutuchokoza...
Taswira rejea hapo juu, baadhi ya matukio duniani wazazi kuuliwa na watoto wao ili warithi mali, wengine kutumia vibaya mali za wazazi na watoto wengine kutokuwa tuu na adabu, utii na heshima kwa wazazi wao kiasi mzazi anaona hivi ya nini nilizaa huyu kiumbe....!!
Majuto Mjukuu, wenzetu (ughaibuni) aidha kwa ugumu wa maisha, sharia zilizowekwa na nchi zao kuhusu matunzo ya mtoto wengine wao wanaona bora kutokuwa na mtoto na badala yake wanakuwa na mbwa wawili au watatu ambapo hao mbwa hawahitaji kupelekwa shule kufundishwa haki za mtoto na saa nyingine kumjibu mzazi atakavyo na kumuitia polisi ikiwezekana (mtoto anampandia mzazi kichwani) na mzazi akifanya fyokoo anapokonywa mtoto na serikali...!!! Balaa.....😌
Wengine wanaona mbwa/paka hatomjibu jeuri, hatokuwa na mawazo kuwa atabadili jinsia kutokana na demokrasia ya dunia n.k n.k.
Dunia inaenda kasi, mambo ni mengi, kuwa na watoto ni jambo nzuri, njema na la kumpendeza Mungu. Ila kulea hao watoto hata waweze kuwa binadamu si jambo jepesi, tumeshuhudia hayo kwa ndugu jamaa na marafiki.
Mbwa anawekewa bili ya msosi maalum, mbwa anatibiwa kila inapohitajika na ana Bima ya matibabu, mbwa analala ndani kwenye nyumba safi, anaogeshwa na kupanda gari la mzazi wake, mbwa anatoka outing na wengine wanapanda nao ndege kwenda safari zao au matembezi..
Kuna waliosema, heri kuzaliwa mbwa ulaya, kuliko.....
Si kuwa mtu wa hivyo amejidharau ama amekata tamaa....
Pengine ni ugumu wa maisha anaopitia wakati akipata taswira huduma anayopata mbwa/paka ulaya hizo hela hao wazazi si wanazichezea tuu... Ila kila mtu na maammuzi yake, ndo ule usemi, usimpangie mtu matumizi ya pesa zake.
Hili jambo limechukua nafasi kubwa sana mashariki ya mbali ukilinganisha na kwetu Afrika.
Wako wa Afrika wanaolea mbwa kama binadamu ila ni wa kuhesabu, huko kwa wenzetu unaweza sema kufuru.
Mbwa/paka ni mnyama rafiki sana kwa mwanadamu, hana baya, unafiki wala husuda au wivu.
Si watu wote wanapenda wanyama wa kufugwa ila dunia inakoelekea.... God knows.
Sina hadidu rejea yeyote kuthibitisha nilichoandika badala yake ni yale niliyoyaona na kushuhudia huku na kule nilikokuwa duniani...
Tembea Uone.....!!😉
Alamsiki.