Kama bado haujaweka Dawa, nakushauri usizianze Hizo dawa japo ndo maamuzi yako yalipofikia.
Nakwambia hivi Labda kwasaabu haujajua madhara yake hasa hasa kwa nywele ambazo kwa wakati huo ziko weak Yaani zinakatika.
Dawa itasababisha nywele yako iwe hatarini zaidi kukatika kwa kuidhoofisha.
Nashauri ununue hair moisturizing cream/lotion for natural hair,pia ufanye deep conditioning with deep conditioner for natural hair,Unaweza kufanya hii hata Nyumbani kwako,alafu upake leave in conditioner Pamoja na hair moisturizer,Unaweza kutumia leave in conditioner Kama moisturizer pia zikiwa bado zina ubichi wa maji, malizia na mafuta.jitahidi hivi kila uoshapo nywele utaona mabadiliko makubwa.
The best kwenye maamuzi yako.