Reli ya kisasa ingeweza kuongeza pato la Taifa maradufu

GwaB

JF-Expert Member
Joined
Mar 19, 2014
Posts
4,291
Reaction score
5,786
Tanzania ilipo,pamoja na rasilimali zake zote tulizonazo ni mtaji unaotosha kabisa kuifanya nchi yetu kuondoka kabisa katika kundi la nchi masikini sana duniani.Fedheha hii ambayo kwa kiasi kikubwa tunailea wenyewe,pamoja na jitihada hafifu zinazonadiwa kama mafanikio makubwa kwa miaka 50,Ingeweza kuondoka kabisa katika kipindi cha miaka kuanzia kumi kutoka hivi sasa kama tungetumia vizuri nafasi ya nchi yetu katika ukanda huu,ambayo ndiyo rasilimali asilia tuliyopewa na Mungu.Tanzania imezungukwa na nchi takriban nane upande wa kaskazini kusini na magharibi.Upande wa mashariki ni mada nitakayoianzisha siku za karibuni.Nchi nane na zaidi sana 9 hazina milango ya bahari na hii ndiyo inayoiweka Tanzania katika nafasi nzuri ya kujenga miundombinu imara kuzihudumia nchi hizi katika kusafirisha bidhaa wanazoagiza nchi za nje na kadhalika bidhaa zao wanazosafirisha kwenda nje kwa kutumia reli na bandali zetu.Reli yetu ya kati ni matokeo ya mkakati wa wajeremani ambao walitaka kutumia neema ya nchi hii ili kujenga uchumi wa koloni lao.Miaka zaidi ya mia tangu ilipojengwa reli ya Dar es salaam-Kigoma wazo hilo bado hadi leo linaweza kutoa matokeo yaleyale kama tukiamua leo kuanza kulifanyia kazi.Kwa bahati mbaya sana,nchi yetu na hasa viongozi wetu tunaowachagua miaka yote wamebakia kutaja rasilimali lukuki tulizo nazo bila kufanya jitihada za angalau kuendeleza hata ile miundombinu ya kikoloni tuliyoirithi.Viongozi wetu,watendaji wetu,tuliowaamini kushika nafasi nyeti za maamuzi kuhusiana na maendeleo ya nchi hii kwa kweli kwa kiasi kikubwa,mpaka sasa niandikapo wametuangusha sana sana.Ningependa kuona nchi hii licha ya kuimarisha reli iliyopo ikijenga reli ya kisasa ya mwendo kasi na ya njia mbili inayotumia umeme,naamini kama tutachagua viongozi wazuri wenye maona na uchu wa maendeleo ya nchi hii inawezekana kabisa.Tunatakiwa kuanza mwaka huu.Mungu ibariki Tanzania.
 

Attachments

  • SNCF.jpg
    33 KB · Views: 55
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…