Rematch: Anthony Joshua Vs Andy Ruiz imetangazwa rasmi

screpa

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2015
Posts
10,857
Reaction score
15,866
Promota wa AJ ametangaza rasmi uwepo wa rematch kati ya mteja wake na Andy Ruiz mnamo Nov/Dec ingawa bado haijajulikana itafanyikia wapi, hii ni baada ya AJ kupoteza pambano lake la kwanza kwa TKO.


WELL, ni muda wa AJ kujiuliza wapi amekosea aweze kurekebisha makosa yake, akipoteza mechi ya pili then his career is over.....
 
Inabidi ajipange haswa bila hivyo atachezea tena kichapo kwa tumbo tumbo ataanza kutakiwa na mabondia wakawaida wa uzito wake ila wasio na mafanikio wakaoshe nyota.

Hata Mfaume mfaume anamtaka AJ
 
In
Haina maana tayari kashaharibu rekodi yake tayari
Kwani kibonge ikitokea kapigwa naye si atakuwa ataharibu rekodi
yake???

Maana ipo kubwa sana, usiangalie rekodi ya kupoteza tu, kuna rekodi ya 'knock outs' ambayo anaweza kuiendeleza nk...

Kupiga kwa Joshua ndo ladha ya ngumi, hivi sasa anangia ulingoni tukiwa hatujui kwamba ataangushwa ama ataangusha mtu.

Hiyo ndiyo maana halisi ya ushindani.
 

Anthony Joshua Wants Rematch With Andy Ruiz Jr.
 
Andy Ruiz Jr aka Destroyer nyota inazidi kung'ara upande wake.

Pambano la juzi dhidi ya Anthony Joshua lilikuwa ni pambano lilimwingizia kipato mara 10 ya ambacho amewahi kukipata.

Ameingiza takribani USD 5 Mil kwenye hilo pambano, wakati kiasi kikubwa alichowahi kupata ni USD 500,000.

Rematch inapangwa kwamba atapata USD si chini ya 10 Mil. Ukiacha add ons.

Tipwa Tipwa anairudisha Boxing kwenye ramani, mimi binafsi nilipunguza kuangalia boxing kwa sababu imepoteza mvuto, watu wanajilinda na kukwepa zaidi ya punching, ila Tipwa Tipwa kanionyesha radha ambayo sikuiona wakati Mayweather anapigana na Manny Pacq, Joshua vs Klitchko, Wilder vs Fury, etc etc.

Na kitendo cha kumshinda Joshua, ukilinganisha na body buildups zao, records na odds walizopewa, Randy kafurahisha watu wengi sana.

Namwombea pambano lake la kurudiana ashinde.

Kuna watu tulikuwa tunasema kwamba Joshua hajawahi kukutana na real tests, na muda wote kambi yake walikuwa wanakwepesha kumpa mapambano yenye uzito, lakini katokea Randy katuthibitishia.

Ama kweli, kurukaruka siyo dawa ya ulimbo.
 
Kibonge yuko fiti sana! Aj tatizo ni mkata pumzi mapema.marudiano atapigwa tena.andy yupo vizuri ,sikuwahi kumjua kabla,baada ya kumbonda AJ ndio nikaingia chimbo kuangalia mapambano yake yaliyopita.yuko safi kiufundi aisee,sina shaka nae na nina hakika hajabahatisha.
 

Hajabahatisha mkuu, ukiangalia fights zake jamaa ni super aggressive.

Na kuna fights anazimaliza mapema sana, na ana pumzi na stamina pia.
 
Kufumba na kufumbua hii mechi itapigwa Mara tatu,ni kupiga pesa tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…