wana jamvi,ninaomba msaada kwa mtu anayejua kuhusu hili lakini kwa kila hoja au ushauri awe na legal authorities..
SWALI: Endapo mshitakiwa wa kosa la jinai (theft) alikamatwa akawekwa chini ya ulinzi wa polisi kwa siku zaidi ya kumi bila dhamana na baadaye kufunguliwa shitaka la wizi mahakamani.kesi inatajwa na kuahirishwa kwa miezi kadhaa kwa sababu upande wa prosecution haujakamilisha ushahidi.baada ya hapo mshitakiwa anaiomba mahakama imuachie huru (To discharge and not to acquit) na mahakama inafanya hivyo.Je, Mshitakiwa huyo atakuwa na haki zipi katika sheria za madhara (Tort law)?