Ameingia Vodacom kawafukuzisha wazembe wote. Watu walikuwa na vyeo vya ajabuajabu na mishemishe za kijanja kazifagilia mbali.
Magari ya Vodacom yalikuwa yamepamba mitaa ya nchi hii. Sasa hivi hesabu mtaani uone kama utakutana na gari zina nembo ya Vodacom. Chache kweli na ni za kuhesabu na hata ukziona ziko choka mbaya.
..Nchi ya kitu kidogo, utajiri wa fasta fasta, ujanja ujanja......Nakulilia Tanzania. Go ahead Rene Meza. Fukuza woote, tuanze upya
Wengi wameacha kazi kutokana na sera yake ya kubana matumizi anayoiita EBIDTA.
Juzijuzi niliona mfanyakazi mmoja wa Vodacom akipanda bodaboda nikauliza kulikoni akanijibu wee wacha tu mambo ni balaa.
Vodacom si mahala pa kukimbilia tena, na mtu akifanya kazi Vodacom mhurunie badala ya kumsifia. Hapafai. Huyu jamaa hafai.