REPOA: 88% ya Watanzania hawawezi kuandamana dhidi ya Serikali

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Utafiti wa Taasisi ya Utafiti REPOA unaonesha Watanzania wana hofu ya kukosa huduma muhimu za kijamii endapo watamchagua kiongozi yeyote kutoka vyama vya upinzani.

Utafiti huo umeonesha kuwa asilimia 88 ya wananchi waliohojiwa walisema hawapo tayari kuandamana kuishinikiza Serikali kuwapatia huduma, huku asilimia 77 wakisema njia watakayoitumia ni kuwasilisha kero zao kwa viongozi wa Serikali za mitaa yao.

Hata hivyo, Mtafiti Mwandamizi wa Repoa, Dk Hubert Shija alisema walibaini kati ya watu wanne, watatu hupendelea kuwa karibu na mtu wa chama kingine cha upinzani lakini mtu mmoja kati ya wanne hajali lolote.

Asilimia 96 ya wananchi wanaamini utoaji wa huduma bora ni jukumu la Serikali na hawaoni muunganiko wa ulipaji wa kodi kubwa na kupata huduma.

Wananchi hao walisema kukiwa na ufanisi wa utoaji huduma na kuwashirikisha viongozi wa kisiasa utoaji wa huduma utakuwa mzuri.
 
Hizi ripoti huwa naona zinaletwa kwa malengo maalum, hasa ya kutuliza joto la kisiasa linapoonekana kuwa limepanda kwa wakati husika, mathalani wakati huu wa kelele za tozo, ndio hao REPOA wanasema 88% ya watanzania hawawezi kuandamana dhidi ya serikali, hizi ni kama "mind games" wanazotuchezea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…