Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,362
- 48,879
Kwenye mazingira ambayo wengi wanalalamikia hali ngumu ya uchumi, na hata katika ugumu huo wanatozwa kodi na tozo, halafu anapatikana wa kula pesa hiyo iliyopatikana kwa taabu, na watoaji wa pesa wakipitia hali ngumu za kimaisha, hasira inakuwa kubwa sana. Na katika hasira, mara nyingi hekima huwekwa pembeni.
Hakuna ubishi kuwa maisha ya Watanzania walio wengi ni magumu sana. Viashiria vya haraka, ukifika tu Tanzania, vinavyoonesha ugumu wa maisha ya uhakika, ni yale unayoweza kuyaona:
1) Kazi zisizo rasmi zimejaa kila mahali, boda boda kila mahali, wauza nyanya na michicha kila mahali, wauza mitumba kila mahali, ukibeba hata kamfuko kenye uzito wa kilo 2 kijana anakuja anataka akusaidie kubeba ili umpe chochote, n.k. Yaani barabara hazieleweki, soko halieleweki, hoteli na migahawa havieleweki maana kila mahali ni magenge ya vyakula.
2) Ukitoa tangazo la kazi, unataka watu wawili, maombi elfu 10, zaidi ya robo wote wana sifa.
3) Kila dakika kwenye radio na TV unasikia matangazo ya michezo ya kubahatisha ambayo inazidi kuwaangamiza zaidi maskini.
4) Waajiri kulipa mishahara midogo sana lakini hawakosi wafanyakazi.
5) Ukidondosha hata leso ambayo thamani yake haizidi sh 2,000 ukirudi baada ya dakika 2 huioni. Na kuna wakati mtu anaweza kuichomoa hata toka mfukoni mwako.
Haya yanaashiria tatizo kubwa la ajira na kipato kidogo sana cha watanzania walio wengi.
Katika dhiki na umaskini mkubwa kama huu, huku kukiwa na mipango duni ya kuongeza ajira na vipato, akipatikana anayetuhumiwa kuiba, kufuja pesa ya umma, lazima hasira za wananchi zitakuwa hazielezeki.
Inafahamika kuwa Watanzania ni wazembe sana kufuatilia haki zao na kuchukua hatua za ki-umma kama maandamano na migomo, lakini udhaifu huu wa wananchi usichukuliwe kuwa ni wa kudumu. Hata bubu pamoja na kushindwa kuongea, mambo yakimzidi ana uwezo wa kupiga kelele, na mbaya zaidi huwezi hata kujua kelele ile ndani yake ina maneno gani, unaweza kuja kushtushwa na vitendo.
USHAURI
1) Rais ndiye mkuu wa nchi. Ndiye anayebeba dhamana yote. Wizi au ubadhirifu kama umefanywa na Waziri, ni Rais ndiye aliyemteua huyo waziri. Wizi ukifanyika kwenye ofisi ya mkurugenzi wa Halmashauri, huyu mkurugenzi ameteuliwa na Rais. Wizi ukifanyika kwenye taasisi na mashirika ya umma, hao wakurugenzi na wajumbe wa bodi, wote ni wateule wa Rais. Wananchi wana haki ya kumlaumu Rais kwa sababu hao wote, siyo wananchi waliomwambia Rais awateua. Aliwateua yeye baada ya kujiridhisha kuwa wanafaa.
Maadamu wateule hawa wa Rais wametenda kinyume, ni lazima Rais awe na lugha ya kuonekana inayosema, "wananchi nilikosea, hawa niliowateua nilidhani ni watu wazuri kumbe ni majambazi". Na kwenye hilo, vitendo ndiyo viongee, na siyo maneno. Kwa hatua atakazozichukua Rais, wananchi waone kabisa kuwa Rais amesikitishwa na uteuzi wa watu hawa. Maneno hayatafaa sana.
2) Rais na Bunge watoe kauli juu ya ratiba na hatua za kuifanyia kazi report ya CAG.
3) Bunge liahirishe mambo mengine yote ili kushughulikia jambo hili la dharula lililoleta taharuki kwa wananchi. Kuendelea kuijadili bajeti ambaye inaenda kuibiwa na hawa wevi ni kupoteza muda. Tushughulikie hatua za kuziba pipa lilitoboka. Kuendelea kujaza maji kwenye pipa ambalo kitako chake hakipo ni kupoteza muda.
4) Wananchi waambiwe, ni lini taarifa ya mwisho itatolewa kwao juu ya nani alifanya nini kwenye upotevu wa pesa uliotokea.
5) Mwisho wa yote, kwa haya yaliyotokea, Waziri Mkuu ajiuzulu ili Baraza la Mawaziri liundwe upya, wale wenye kashfa waachwe na hatua nyingine ziendelee dhidi yao.
6) Itungwe sheria inayotamka kuwa Waziri, Mkurugenzi wa taasisi yoyote ya umma au Halmashauri, endapo wizara yake au taasisi yake au Halmashauri yake, kukitokea upotevu wa pesa ya umma, na yeye hakuchukua hatua yoyote, au kama yeye mwenyewe alihusika, atafukuzwa kazi na hataruhusiwa kugombea nafasi yoyote ya uongozi, wala kuteuliwa au kuajiriwa Serikalini au taasisi yoyote ya umma.