TANZIA Rest In Peace John Makelele a.k.a Zig Zag aliyemtungua Sahau Kambi 1988 na Simba kunusurika kushuka daraja

Mwishokambi

JF-Expert Member
Joined
Nov 23, 2020
Posts
390
Reaction score
1,425
Nimepata taarifa za kuhuzunisha juu ya kufariki kwa mshambuliaji hatari wa zamani wa Simba John Makelele Zig Zag pale Muhimbili juzi jioni.Kwa wale mliozaliwa miaka ya 2000, ni Makelele ndio alitunusuru kushuka daraja mwaka 1988 baada ya Sahau Kambi, kipa hatari wa Yanga mzaliwa wa morogoro kuudaka mpira halafu akawa anamletea utani Makelele, ilikuwa dakika kama ya 56 au 57 wakati huo bao ni 1 kwa 1, marehemu Edo Chumilla ama wonder boy aliwaua yanga dakika ya 12 tu, marehemu Issa Athuman akasawazisha dakika ya 36, hadi mapumziko ilikuwa ngoma droo.

Simba walikuwa na hali na mbaya sana siku ile, wakati huo kulia yanga alikuwa marehemu Yussuf Ismail Bana na kushoto alikuwa yanga lia lia Fred Felix Minziro, Minziro alicheza kwa uchungu sana siku ile, Simba walikuwa wanahaha kutafuta goli la ushindi ili wasinusurike kushuka daraja,.sasa Sahau Kambi akawa analeta utani utani, anadaka mpira anacheza nao, Makelele alikuwa na njaa sana, Simba ilimtoa Mwanza akiwa Pamba FC, alikuja Simba akiwa na Dan Mhoja marehemu pia.

Ilipofika dakika ya 58 Sahau Kambi akiwa amedaka mpira huku akijua kabisa Makelele anammezea mate, akaanza kuuchezea chezea, katika kuuchezea ukamponyoka bana, hapo kosa bila ajizi Makelele aliuwahi mpira na kuukwamisha wavuni mara moja, alifunga goli hilo upande wa kaskazini wakati huo enzi hizo sisi vijana tulikuwa tunaruhusiwa kuingia bure uwanjani.Pale ilipojengwa uwanja wa sasa hivi kuna sehem ilianguka ndege ndio sehemu tuliyokuwa tunapita tukitokea chuo cha ualimu sasa hivi Duce tunazama kwenda uwanjani, ukuta ulikuwa mfupi sana kiasi kwamba wahuni wa keko na chang'ombe walikuwa wanaweza kuruka na kuzama ndani fasta, enzi hizo kulikuwa na farasi na ninamkumbuka sana afande Marboro akiwa na farasi, mbwa ndio ilikuwa usiseme, wafanya vurugu wote walikabiliana na mbwa.

Wengine tumetoka mbali sana katika mpira, tunapoweka mada hapa muwe na adabu, mimi namheshimu sana Gentamycine kwa sababu ndie anaenithibitishia kuwa mpira hakuanza kushabikia Leo.Tumeziona Nyota Nyekundu ya Roster Ndunguru, Pilsner ya Said Mrisho Zico wa Kilosa, Yanga ya akina Edgar Fongo, Sigara ya akina Rashid Mmanda.

Nawaombea kwa mwenyezi mungu wote waliotangulia mbele ya haki, R.I.P John Makelele Zig Zag.
 
Heshma yako mkubwa.
ahasante sana kumbukizi.[emoji120]
 
Dah! Umenikumbusha mbali mkuu. Wakati huo redio ni Moja mtaa mzima mnakusanyika kusikiliza mpira.

Ikitokea timu ya mwenye redio ikafungwa jamaa anazima redio watu mnasambaa. Mkisambaa yeye anafungua redio anaenda kusikilizia chumbani. Wakisawazisha anarudi nje halafu anawaita tena mje kusikiliza.
 
Dah! Umenikumbusha mbali mkuu. Wakati huo redio ni Moja mtaa mzima mnakusanyika kusikiliza mpira.

Ikitokea timu ya mwenye redio ikafungwa jamaa anazima redio watu mnasambaa . Mkisambaa yeye anafungua redio anaenda kusikilizia chumbani. .Wakisawazisha anarudi nje halafu anawaita tena mje kusikiliza.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] khaaaaah
 
Dah! Umenikumbusha mbali mkuu. Wakati huo redio ni Moja mtaa mzima mnakusanyika kusikiliza mpira.

Ikitokea timu ya mwenye redio ikafungwa jamaa anazima redio watu mnasambaa . Mkisambaa yeye anafungua redio anaenda kusikilizia chumbani. .Wakisawazisha anarudi nje halafu anawaita tena mje kusikiliza.
[emoji3]
 
Nadhani hii habari itakuwa sio sahihi sana!!!!

JOHN MAKELELE alifariki zamani sana (kama sikosei) Tena wametoka kijiji kimoja ama vijiji jirani na alikuwa jambazi maarufu WILLY WHITE (Huko pembezoni mwa ziwa Nyasa)
 
JOHN MAKELELE, EDWARD CHUMILA, MALOTA SOMA, ISSA KIHANGE, TWAHA HAMIDU, DEO NJOHOLE, MOSES MKANDAWILE, RAPHAEL PAUL, ALI MACHELA.........
 
Nadhani hii habari itakuwa sio sahihi sana!!!!

JOHN MAKELELE alifariki zamani sana (kama sikosei) Tena wametoka kijiji kimoja ama vijiji jirani na alikuwa jambazi maarufu WILLY WHITE (Huko pembezoni mwa ziwa Nyasa)
Nimeshangaa kabisa John Makelele alifariki Kitambo sana akiwa Milambo ya Tabora.
 
Makelele alikuwa akifanya kazi CRDB hadi anastaafu, ameacha watoto 5, huyo anayesema amefariki kitambo, aisee
 
Nimepata taarifa za kuhuzunisha juu ya kufariki kwa mshambuliaji hatari wa zamani wa Simba John Makelele Zig Zag pale Muhimbili juzi jioni.Kwa wale mliozaliwa miaka ya 2000, ni Makelele ndio alitunusuru kushuka daraja mwaka 1988 baada ya Sahau Kambi, kipa hatari wa Yanga mzaliwa wa morogoro kuudaka mpira halafu akawa anamletea utani Makelele, ilikuwa dakika kama ya 56 au 57 wakati huo bao ni 1 kwa 1, marehemu Edo Chumilla ama wonder boy aliwaua yanga dakika ya 12 tu, marehemu Issa Athuman akasawazisha dakika ya 36, hadi mapumziko ilikuwa ngoma droo.

Simba walikuwa na hali na mbaya sana siku ile, wakati huo kulia yanga alikuwa marehemu Yussuf Ismail Bana na kushoto alikuwa yanga lia lia Fred Felix Minziro, Minziro alicheza kwa uchungu sana siku ile, Simba walikuwa wanahaha kutafuta goli la ushindi ili wasinusurike kushuka daraja,.sasa Sahau Kambi akawa analeta utani utani, anadaka mpira anacheza nao, Makelele alikuwa na njaa sana, Simba ilimtoa Mwanza akiwa Pamba FC, alikuja Simba akiwa na Dan Mhoja marehemu pia.

Ilipofika dakika ya 58 Sahau Kambi akiwa amedaka mpira huku akijua kabisa Makelele anammezea mate, akaanza kuuchezea chezea, katika kuuchezea ukamponyoka bana, hapo kosa bila ajizi Makelele aliuwahi mpira na kuukwamisha wavuni mara moja, alifunga goli hilo upande wa kaskazini wakati huo enzi hizo sisi vijana tulikuwa tunaruhusiwa kuingia bure uwanjani.Pale ilipojengwa uwanja wa sasa hivi kuna sehem ilianguka ndege ndio sehemu tuliyokuwa tunapita tukitokea chuo cha ualimu sasa hivi Duce tunazama kwenda uwanjani, ukuta ulikuwa mfupi sana kiasi kwamba wahuni wa keko na chang'ombe walikuwa wanaweza kuruka na kuzama ndani fasta, enzi hizo kulikuwa na farasi na ninamkumbuka sana afande Marboro akiwa na farasi, mbwa ndio ilikuwa usiseme, wafanya vurugu wote walikabiliana na mbwa.

Wengine tumetoka mbali sana katika mpira, tunapoweka mada hapa muwe na adabu, mimi namheshimu sana Gentamycine kwa sababu ndie anaenithibitishia kuwa mpira hakuanza kushabikia Leo.Tumeziona Nyota Nyekundu ya Roster Ndunguru, Pilsner ya Said Mrisho Zico wa Kilosa, Yanga ya akina Edgar Fongo, Sigara ya akina Rashid Mmanda.

Nawaombea kwa mwenyezi mungu wote waliotangulia mbele ya haki, R.I.P John Makelele Zig Zag.
Ukieleza ukweli utachomwa kisu? Kuna Mtu kakushikia kisu hapo hadi uanze kusema Uongo? Kama kweli ulikuwa unajitambua;
1. Nani alikuwa REFA wa hiyo mechi maana ni maarufu sana.
2. Mbona hujaeleza Yanga angeshinda au angedroo angekuwa nani?
 
Dah! Umenikumbusha mbali mkuu. Wakati huo redio ni Moja mtaa mzima mnakusanyika kusikiliza mpira.

Ikitokea timu ya mwenye redio ikafungwa jamaa anazima redio watu mnasambaa . Mkisambaa yeye anafungua redio anaenda kusikilizia chumbani. .Wakisawazisha anarudi nje halafu anawaita tena mje kusikiliza.
Hee😂😂😂🙌
 
Back
Top Bottom