Retrenchment

Retrenchment

kimwelage

Member
Joined
Oct 13, 2012
Posts
55
Reaction score
21
Boss wangu alinijulisha kwa mdomo kwamba natakiwa kuwa rentrenched kwa hiyo HR watanijulisha Zaidi. Siku mbili baadae, nikapewa Termination Letter ambayo inasema ajira yangu itakoma baada ya siku 28.

Nataka kujua unaweza kuwa terminated bila kufuata taratibu na bila kupewa sababu
 
Mimi si mwanasheria ila ukienda Ofisi za Kazi na Ajira bosi wako atakupigia magoti. Atakulipa Mshahara wa Mwaka Mzima na marupurupu yake walahi.

Je Nini sababu ya Retrechment? Mwajiri pia anapaswa kufahamu kuwa Hana ruhusa ya kuajiri mtu mwingine katika nafasi yako kwa kipindi kisichopungua miezi 6 Kama ni Retrechment.

Wengine wake wachangie.
 
" Siku
mbili baadae, nikapewa
Termination Letter ambayo
inasema ajira yangu itakoma
baada ya siku 28 "

Bado hapajakuwa na tatizo hapo. Ikisha koma ndio utajua, maana possibly huenda package yako inaandaliwa ukabidhiwe
 
Kwani mkataba wako wa ajira upoje?? Ni ajira ya kudumu na penshen ya uzeeni au ya mkataba wa muda fulani?
 
Nashukuru huu mjadala nimeuwahi ebu twende haraka haraka hapa tutatumia sheria mbili moja ELA (Employment and labour relation act 2004) kiswahili chake ni sheria ya ajira na mahusiano kazini ya mwaka 2004 na ile tunaita code of good practice 2007 kingereza na kiswahili tunaita kanuni za utendaji bora.

Tuanze sasa sheria ya ajira na mahusiano kazini inasema kuna sababu 4 za ajira kufika mwisho ikiwemo
1. mahitaji ya kiundeshwaji yani retrenchment or operation requirement
2. Mwenendo mbovu yani kingereza chake Misconduct
3. Incapacity maana yake utendaji kazi usio ridhisha au mbovu
4. incompatibility hii tunaita kuendana

Haya sasa hizo sababu zinapatikana kifungu cha 37 sheria ya ajira na mahusiano kazini

sasa narudi kwenye iyo ground yako ambayo inasema retrenchment na utaratibu wake upoje na stahiki zako unazostahili kama mfanyakazi.

Kifungu cha 38 cha sheria ya ajira na mahusiano kazini muajiri akitaka kukupunguza kazini anatakiwa kutoa taarifa maana kifungu cha 41 kipo wazi kinamtaka kutoa taarifa ya siku 28 hivyo hapo yupo sahihi

pia lazima atoe sababu za upunguzaji huo na jitihada zake alizofanya kuokoa iyo hali
ila penye utata ni hapa ni njia ipi aliyotumia kupunguza maana kuna LIFO and FIFO kuna ile tunaangalia nani wamekaa mda mrefu kwenye kampuni ndo tutaanzia hao hao

Tuje kwenye stahiki zako utazopewa na ndio haki yako kwa mujibu wa kifungu cha 44 katika sheria ya ajira na mahusiano kazini ya mwaka 2004

1. Siku ulizofanya kazi
2. likizo kwa mujibu wa kifungu cha 31 amabzo zitakuwa ni siku 28
3. malipo ya notisi kama kifungu cha 41 kinavyosema ila sasa wewe hutopewa kwa kuwa ulishapewa taarifa siku 28 kabla
4. malipo ya kiinua mgongo kama kifungu cha 42 kinavyotaka ila usifikiri kiinua mgongo ni pesa nyingi huwa inafanyika hivi mfano mshahara wako wa siku ni 10,000 watazidisha na saba na idadi ya miaka uliyotumikia kampuni mfano umetumikia mwaka mmoja tutapiga 10,000*7*1 maana yake kiinua mgongo ni elfu 70,000 angalizo ukipunguzwa kazini hata kiinua mgongo haupati na sheria ipo wazi ila labda muajiri awe na huruma tu.
4. Kama uliajiliwa dar ukapelekwa rukwa utapewa nauli ya kurudi dar
5. utapewa cheti cha utumishi bora ulitukuka

labda hapo kama una nssf za kutosha zitakufuta machozi usishitaji wa ajira wenye manufaa ni ule wa makubaliano hapo ndo pesa ipo yani tunaita termination by agreement
 
Wanasema ni kupunguza wafanyakazi kutoka na mapatao kuyumba
kama unampunguza mfanyakazi kutokana na mapatano - inaitwa Termination by Agreement
Ila kama unamuondoa au kumpunguza mfanyakazi kwa sababu za kiuchumi au kuyumba kwa mapato kama ulivyoandika- Retrenchment
Rentrenchment na Termination by Agreement ni vitu viwili tofauti na hata taratibu za kusitisha mkataba au ajira ya mfanyakazi zinatofatiana
 
Termination by agreement Huwa inatofautiana vipi na hizi zingine?
 
Termination by agreement Huwa inatofautiana vipi na hizi zingine?
hizi huwa mfanyakazi na kampuni wanakaa mezani kumaliza uhusiano wa ajira kwa maridhiano mfano mkataba unaweza kuwa umebakia miezi 9 ila kuna namna kampuni inakuwa haikuhitaji ila sasa kusema moja kwa moja wanakuwa hawana sababu za wazi hivyo wanakuita mumalizane sasa nini kinajadiliwa hapo kwanza kampuni itakuambia hii miezi 9 iliyobaki labda tutakulipa mishahara ya miezi 7 ongeza na likizo na kiinua mgongo mkishakubaliana labda jumla mil 10 ndo mnasign sasa kitu kinaitwa Termination by agreement settlement of disputes hapa mashahidi wa pande zote 2 wanakuwepo ili kuleta tija nikitulia ntaleta sample ya hayo makubaliano yapaswa kuwaje

katika sababu au namna ambayo mfanyakazi anaondolewa kazini njia ya makubaliano huwa inamnufaisha sana mfanyakazi maana mara nyingi anayetakaga mkae mezani ni kampuni hapo ndo ukute mkataba umebakia hata miaka 2 kama ambavyo bwana ronado aliondoka pale manchester united ni kwa makubaliano ya pande 2 au robetihno wa simba au kama sahivi Simba wasingeomba radhi kwa chama wangemalizana kwa makubaliano
 
kama unampunguza mfanyakazi kutokana na mapatano - inaitwa Termination by Agreement
Ila kama unamuondoa au kumpunguza mfanyakazi kwa sababu za kiuchumi au kuyumba kwa mapato kama ulivyoandika- Retrenchment
Rentrenchment na Termination by Agreement ni vitu viwili tofauti na hata taratibu za kusitisha mkataba au ajira ya mfanyakazi zinatofatiana
Mkuu hapo kwenye Retrenchment kama Boss Sababu zake za kukupunguza ni kuwa Uchumi umeyumba Ila kiuhalisia haiko hivyo Ila ni chuki zake tu binafsi (Personal Grudges) Sheria inasemaje kuhusu hili?
Maana anakupunguza then anaajiri mwingine,anapunguza mwingine then anaajiri tena mwingine and so and so kwa hili Sheria inasemaje hâta baada ya kujiridhisha kuwa Uchumi si sababu ya kufanya apunguze..
 
Na ndo mchezo wao
 
pole sana,navyofahamu kama mwajiri atapunguza wafanyakazi kw sababuza kiuchumi basi hataweza kuajiri wafanyakazi wengine katika Idara hiyo hiyo angalau hadi kipindi cha miezi 6 kipitie,lakini huwezi sema unapunguza wafanyakazi alafu kwa wakati huo huo unaajiri wafanyakazi wengine na huenda wakawa wanalipwa mshahara mkubwa au kama ule ule waliokuwa wanalipwa watangulizi wake.
Kukiwa na mazingira hayo basi sababu ya kupunguza wafanyakazi haikuwa sahihi na halali,ndio maana kabla ya kufikia hatua ya kupunguza wafanyakazi kuna taratibu za kufuatwa,pia lazima aweze kuonyesha kuwa hakuwa na mbadala mwingine wa kupunguza madhara ya uchumi katika biashara yake zaidi ya kupunguza wafanyakazi,na mbdala huo ni kama KUPUNGUZA MISHAHARA kwa wafanyakazi.
Ila usisahau utafuta ushahidi wa Mwajiri /kampuni kuajiri watu wengine baada ya wewe kupunguzwa kazi
 
Back
Top Bottom