Revenge: Napeleka kilio kwa binti fulani siku ya kupeleka barua

daah naona mzee umeandika kwa uchungu mno.. polee sanaa.. kamwaga mboga we mwaga ugali vunja na bakuli kabsaa
 
MREJESHO....

Naomba kwanza niwaombe radhi wote mliokuwa mnasubiria mrejesho hadi mkachoka, niwashukuru pia wale waliokuja PM kunishauri na polen maana ushauri wenu haukuzingatiwa.

Tarehe 07 january kila mwaka itakuwa ni siku yangu ya kumbukumbu.

Kwanza nianze kwa kusema kisasi ni haki ya mtu aliyefanyiwa ubaya pasipo yeye kufanya ubaya, siku tajwa hapo juu ni siku niliyeachana na mwanamke wangu ambaye ndo tulikuwa kwenye hatua muhimu za kuoana, mwanamke aliyenifanyia ushenzi wa kishenzi na mim nikawa sina namna zaidi ya kumfanyia ushenzi wa kishenzi kama yeye.

Siku ilianza vema kwa safari ndefu kuelekea kwa wazazi wake, nikiwa na mshenga na mzazi wangu na baadhi ya ndugu, njian stori zilikuwa za kunipongeza kwa kuchukua uamuzi huu wa kuoa, wakati wote mim nilikuwa kimya nikizid kutafakari zaid jinsi nitakavyopeleka kilio kikuu kwa yule binti, nikiri kwamba nilifikiria pia kuhusu wazazi wake na wangu pamoja na ndugu, jamaa na marafiki watakaokuwepo ila bad luck ni kwamba option ilikuw moja tu.

Majira ya saa 2 hv usiku tukawasili nyumbani kwa binti, tulipokelewa kwa bashasha na shamra shamra sana, tukapikiwa chakula kisha tukapelekwa sehemu ya kupumzika na kesho saa 4 asubuhi ikawa ndo muda muafaka wa tukio la mahari ili pia sisi tuweze kurudi mapema.

Asubuhi ilikucha vema sana, nikiwa nimeprint messages zote na zile picha tayari kwa kumpiga mtu tukio, muda wa kwenda sehemu iliyoandalia ya mazungumzo ukafika, kama mnavyojua muoaji huwa anaitwa mwishoni baada ya wazee kukabidhiana mahari waliyokubaliana, ikabidi mimi niombe kuvunja utaratibu kwa kuomba niwepo kwenye kutoa mahari hiyo km haitakuwa shida sana, mshenga akasema sio shida inawezekana tu, kweli niliruhusiwa na mshenga akapiga maneno maneno pale ikawa uwepo wangu pale wala sio shida.

Baada ya kukaribishwa na upande wa kikeni ukafika muda wetu sasa wa kujimwambafy kwa kutoa mpunga then taratibu zingine zifuate hapo mim nikainterven kwa kuomba niongee kdg, baba wa binti akasema niruhusiwe maana ile ni kwa ajili yetu, basi nikaomba binti aitwe pale kwenye kikao, ni km walitaka kudadisi kitu ila mim nikaomba binti aje kabla hatunaendelea, niliongea politely sana wala sikuwa na hasira, binti akaitwa na kumbe alikuwa kwenye kuandaa chakula hivyo ikabidi akimbie bafun faster kisha akaja.

Pamoja na wazazi wa binti lakin pia kulikuwa na wajomba, baba wadogo shangazi yake mmoja na kaka zake. Sikua na maneno mengi nikasema straight tu, nimeghairi kuoa na mahari isilipwe na nimeona niliseme hili mbele ya binti na kikao hiki kikubwa ambacho kinahusisha familia zote mbili, watu wakabaki na butwaa, walitaman kuhis nimechanganyikiwa lakin kwa jinsi nilivyokuwa naongea ikabid wafute hayo mawazo, wakawa buzy sasa kunisikiliza.

Nikamwita binti kwa jina lake, nikamuomba binti aweke wazi kila kitu pale kuhusiana nayeye kuwa na mwanaume mwingine, mama wa binti jasho likamtoka akaanza kumuuliza binti yake km ni kweli alikuwa anafanya ushenzi ule, binti akakana akasema sio kweli na hajawahi kujihusisha na mwanaume yeyote tangu nimchumbie huku machozi yanamtoka akaanza kuapa kwa majina yote ya mungu wake, akaanza kujifanya anataja vifungu vya biblia, asee walokole ni wanafiki nafiki sana.

Kikao kikawa kimebadilika sura, kila mtu akabaki ana hamu ya kuujua ukweli, mshenga akaniita tutoke nje kidogo nikakataa, nikamwambia binti aache kupretend aseme ukweli, akaendelea kukataa pale, basi baba wa binti akasimama akasema yeye km mzazi wa binti na mkuu wa ile familia ile ni aibu kubwa na km nitashindwa kuthibitisha basi ataenda kwenye vyombo vya sheria kudai fidia ya binti yake, kwanza ya kumpotezea muda na pili ya kumdhalilisha na kumuumiza kisaikolojia binti yake.

Baada ya kuona binti anakomaa kwamba sio kweli na mzee wangu akawa yupo tu haelewi aseme nini sasa, nikazama kwenye begi na nikatoa picha na printing za screenshots za msg, nilikuwa nazo za kutosha, nikamkabidhi mzee wake nyingine nikampa yeye mwenyewe na zingine mshenga wangu, nikamwambia aendelee kubisha sasa, kukawa kimya kwa muda baadaye binti akakosa nguvu akaanguka na kuzimia, ikabidi akambizwe hospital.

Baba yangu alinilaumu sana kwa kitendo kile, hata mshenga akasema nilitakiwa niseme mapema tungepiga simu tu kwamb tumeahirisha kuliko nilichokifanya, nikawajibu tu moyo wangu usingeridhika kufanya kirahis vile lakn pia binti angepata nafasi ya kuwaongopea wazazi wake na wangemwamin kwa kuwa ni binti yao, namim kwa wazazi wa yule binti ningebaki kwenye kumbukumbu mbaya milele, nikawaomba wanielewe tu hakuna namna.

Ikapangwa jion tuwe ni kikao tuone nini kinafuata sasa.

ITAENDELEA...

Mrejesho: Sehemu ya pili
 
Fanya haraka mzeeya iendelee!!!

Sent from my Infinix X572 using JamiiForums mobile app
 
Hii nataka niiweke kwenye kitabu nipe muongozo mkuu
 
TUENDELEE..

Jioni ile binti alizinduka, lakin Daktari akaomba binti abaki wodin maana mapigo yake ya moyo hayapo vizuri na presha ipo juu kupita maelezo, lakin kutokana na nature ya tatizo lenyewe ni bora binti abaki kwa uangalizi na counseling maana anaweza kuchukua maamuzi mabaya, binti akabaki hospital na mama yake, wengine wakarudi home. Jioni ikafika kikao kikaitishwa.

Baba wa binti akaongea mengi km kunilauma mim, nikaon ananiletea uhuni, nikamchana kwamba nilishamweleza kwamba akifanya ushenzi namim nitafanya ushenz na hizo msg kwenye simu zipo na kama binti atakataa nazionesha vile vile jinsi tulivyokubaliana, basi ikabid busara zitumike, hasa mjomba wake ambaye alijitahidi kutuomb radhi kwa binti yao kukosa maadili kiasi kile japo limekuja wakat mbaya lakin lmesaidia sana kuelewa uhalisia wa binti yao ambao walikuwa hawaujui.

Baada ya dk kidogo mama yake akaja kutoka hospital akatukuta kwenye kikao, akaomba sana niende hospital nikamuone binti yake maana hakuna anachotaka zaid ya mimi na hayupo tayari kuishi km sitamsamehe, akaniomba sana niende hospital nikamtamkie msamaha hata wa kinafiki, nikakataa na sikwenda, nikawaambia wazee tusepe hapa hakuna jipya tena, hapakuwa na jins maana nilikaza kila kona, moyo wangu kwa dhati ulikusudia kulipa kisasi.

Nikatoka nje nikawaacha wazee wakiongea ongea, usiku ulikuwa umeshaingia tukaingia kwenye gari safari ya kwenda hom ikaanza.

Nyumban taarifa zilikuwa zimeshafika, kuna ambao waliona sawa na kuna wajinga na dhaifu wakasema ningesamehe tu nimuoe, wapuuzi.

Maisha mapya yalianza, siku moja nikawa nipo porini huko kwenye mishe zangu zikiwa zimepita km siku 4 hivi nikapigiwa simu na mtu aliyejitambulisha kwamba ni mwasaikolojia, akanambia kuhusu lile tukio na kwamba anaomba niongee na yule binti chochote kwa kuwa hataki kula na muda wote anachungwa maana anaonesha dalili zote za kutafuta namna ya kujinyonga, nikakataa. Nikamwambia aachane namimi kabisa.

Simu zilikuwa nying, mama yake, baba, na ndugu zake wengine lakin sikuwa na mpango tena, nikaona nibadili laini za simu zote. Nikajua nimesolve tatizo sasa, of course wakawa wanaongea na mzee wakiomba aongee namim niongee chochote na binti yao, nikakataa. Miezi kadhaa ikapita, siku moja nikiwa Tanga huko nikapokea simu ya rafik yangu akanijuza kwamba yule binti amekuja ghafla kwake, amekonda na kuchakaa. Kumbe alikuwa ametoroka kwao ili aje anitafute, alikuja kwangu kukawa kumefungwa akaona aende kwa mshikaji.

Nikamwambia kifupi tu, aishi naye pale kwake km anamhitaji ila mim kwa upande wangu ni hapana, jamaa akasema ameoa na ana familia so nafasi pale kwake ni ndogo na binti hataki kuelewa na amekataa kutoka pale kwake akaniomba niongee na yule binti, nikakataa.

Kumbe yule binti aliiba hela za baba ake dukan maana baba ake aliamua kumuweka auze duka la jumla la vifaa vya ujenzj ili angalau apunguze mawazo, akatoka na million 4 akatoroka na kuja kwa mshkaji, akakatalia kutoka hadi anione.

Jamaa akanisimulia mengi kwa kadri binti alivyomuelekeza, Na akaniomba nionane naye ili nimsaidie, nikakataa

Baada ya kukaa km wiki pale jamaa akashindwa ikabid amfukuze kwa nguvu, binti akaamua asafiri aende kwetu kwa wazazi wangu. Muda wote huo kwao hawajui binti yupo wapi, wakaenda kutoa taarifa polisi..

ITAENDELEA WAKUU.

Mrejesho: Sehemu ya tatu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…