Revenge: Napeleka kilio kwa binti fulani siku ya kupeleka barua


Umemaliza yote[emoji1488][emoji1488]
 
Mrejesho
 
Nipo tayari hata kunyongwa km nimefanya kosa la kustahili kunyongwa na nakuhakikishia sitajitetea, nishapoteza pesa zaid ya million 80 kwa kosa langu dogo sana, nipo accountable kwa makosa yangu. So km kuna siku ikitokea nimekosea nipo tayari kwa adhabu yoyote ninayostahili.
 
TUENDELEE...

Baada ya binti kufika kwa wazazi wangu, akajieleza jinsi anavyopata shida na hawezi kuishi bila mimi, jinsi malengo yake yalivyokufa na maisha yake yalivyobadilika. Mzee akanipigia simu na kunieleza ujio wa yule binti pale nyumbani, nikamwambia ampeleke polisi arudi kwao sina muda wa kupoteza kuongelea kitu ambacho jibu lake linajulikana.

Mzee na Bi mkubwa wakaniomba sana niende pale home tukaongee, kwa heshima ninayowapa wazazi wangu ikabidi niende, mzee akawasiliana na wazazi wa binti kuwapa taarifa kwamba binti yao yupo pale, mama wa binti akajipanga kuja kumuona bint yake, baada ya siku 2 nikaenda hom, nikakuta mama wa binti yupo pia, baada ya kufika binti akaanza kuangua kilio akisistiza asemehewe, akaomba km itashindikana kbs basi aishi namim km mfanyakazi wangu hata wa ndani, alikuwa anaongea upuuzi.

Tukawa na kikao kifupi, nikaongea wazi kwamba ukurasa wa yule binti nimeufunga, hana nafasi tena kwangu kwahiyo mama amchukue mwanae arudi naye kwao, akaolewe na wengine huko ila kamwe haiwezi kuwa mimi, hapakuwa na jinsi zaidi ya kukubaliana na msimamo wangu, mama yake akaomba basi niwe angalau naongea na binti yake japo awe ananiskia, nikaona ni ujinga wa hali ya juu mimi kufanya hivyo, nikakataa kufanya huo upuuzi.

Kwa shida shida binti ikabidi aondoke na mama yake kurudi kwao, lakin bado hakua na amani, wakat anaondoka pale alijua nipo Tanga na nafanya kazi na taasisi gani. Alipofika kwao bado hakuwa na utulivu wakat wote alikuwa analia na alipoteza hamu ya kula, akazidi kukonda, habari ile ilikuwa pia imeenea kwahiyo aibu nayo ikawa inamtesa, nikarudi zangu Tanga kuendelea na majukumu mengine.

Mzazi wa yule binti aliongea na mzee akapata namba yangu ya simu akawa ananipigia na kuniomba sana nimsamehe mwanawe maana maisha ya binti yake yamebadilika na yeye km mama anajiskia vibaya sana, akaomba niseme hata kiasi cha pesa ili akilipe km fidia ya ufusika wa binti yake, nikakataa. Akawa ananipigia simu mara kwa mara na ananisistiza kwamba amefanya kila kitu kuhus binti yake lakn hakuna improvement na hakuna namna ya binti yake kuwa sawa zaidi ya mimi kuwa naye karibu.

Nikawa naona ananipigia kelele, sirudigi nyuma, maisha yakaendelea. Nikiwa Tanga naendelea na majukumu yangu nikapigiwa simu na baba wa binti, akaniomba niseme nilipo ili aje tuongee ana kwa ana km wanaume, nikakataa, nikamwambia aongee kwa simu tu tena dk chache, akaniomba kiume kwamba habari za kumuoa binti yake najua haiwezekani tena lakin wao km wazazi wananiomba niwasaidie kt kumfanya yule binti awe sawa, maana wao wamefany kila kitu lakn imekuwa ngumu kwa binti kuwa sawa, nikaona upuuzi, hainihusu chochote. Nikamkatalia.

Ikapita miezi km 3 hv nikiwa tu napokea msg mara kwa mara kutoka kwa wazazi wa binti, nikawa sizijibu. Baadaye nikaoata mapumziko ya kama wiki 2 hivi nikarudi dsm kupumzika. Wiki ya kwanza ikaisha vizuri ila wiki ya 2 ya mapumziko nikapata ugeni pale hom kwangu, ni aliyekuwa rafiki wa karibu na binti, alisema alikuwa anakuja mara kwa mara pale hom kunibahatisha maana hata namba za simu zilikuwa hazipatikani so safari hii ameshukuru kunikuta, akaomba tuongee, nikamwambia poa.

Kwa kuwa nilitoka muda mrefu sana hom, nyumba ilikuwa chafu sana, akafanya usafi akapika, tukiwa tunakula mazungumzo yakaanza...

ITAENDELEA.

Mrejesho: Sehemu ya nne
 
nyuzi kama hizi nazikubali sanaaaa Kumbe wenye maamuz magumu tupo wengi na sio mimi tu[emoji1732][emoji1732][emoji1732][emoji1732][emoji1732] Shusha nyuzi mkuu tuonjoy
 
Kwahiyo Mungu aache kumlipua binti mzinzi aje kumlipua bahati wa watu aliyepanda kweli?

Mungu ni wa double standard kihivyo?

#YNWA
 
Just wondering km Mwenyenzi Mungu angekua mgumu kutusamehe km ww unavyotia ugumu ingekuaje?
Una moyo Mgumu like you have never sin, and sad enough you are proud of it.
Hii sio revenge anymore huu sasa ni ukatili.
 
Hoyaa hii ITAENDELEA ndio nini?
Toa ANDIKO MOJA basi maliza yotee.

#YNWA
 
Just wondering km Mwenyenzi Mungu angekua mgumu kutusamehe km ww unavyotia ugumu ingekuaje?
Una moyo Mgumu like you have never sin, and sad enough you are proud of it.
Hii sio revenge anymore huu sasa ni ukatili.
Wakati dada anatoa Tigo HAKUJUA kuwa anamuumiza baharia anayemuhudumia kwa kila kitu?

#YNWA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…