Reviews za volkswagen touareg 2.5 tdi sport 5dr diesel engine

Reviews za volkswagen touareg 2.5 tdi sport 5dr diesel engine

Pafyum

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2012
Posts
208
Reaction score
113
Habari wataalamu

Naipenda sana Volkswageni Touareg 2.5 Diesel Engine especially ya mwaka 2004 (maana latest Kodi yake siiwezi). Naomba kupata reviews kwa wataalamu kuhusu ubora wa gari hii, performance power, fuel consumption na kila kitu ambacho mtu ana uzoefu na gari hii. Natanguliza shukrani zangu za Dhat
 
Humu wengi wana uzoefu na magari ya Toyota. Ungeleta Vitz, thread yako ingeshafikisha Replies mia!
 
Pia, nshakwambia kwenye uzi wako ule mwingine. Achana na Touareg. Gari za mzungu huwa zinachemka huku Africa. Kuna mzungu katelekeza Touareg yake pale Mwenge huu mwaka wa tano! Bora uchukue Discovery 3.
 
Gari ya mwaka 2004 unaulizia kuhusu ubora wake? I mean hiyo gari ina miaka 15 sasa iweje iwe bora? Hapo kila kitu kimeshakwisha tayari.
 
Gari ya mwaka 2004 unaulizia kuhusu ubora wake? I mean hiyo gari ina miaka 15 sasa iweje iwe bora? Hapo kila kitu kimeshakwisha tayari.
Kwani hizi gari mnazonunua huko kwenye mayard unafikiri ni za mwaka gani? Nyingi ni 2005 kwenda chini. Tulipaswa kujiuliza wenzetu wanatunzaje magari? Gari ya mwaka 2000 sisi tuziita mpya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Touareg naikubali sana hio gari ni pesa tu hazijachanganya vizuri. Wanadai version za mwanzo zina mauza uza mengi.
 
Gari ya mwaka 2004 unaulizia kuhusu ubora wake? I mean hiyo gari ina miaka 15 sasa iweje iwe bora? Hapo kila kitu kimeshakwisha tayari.
Kumbe hujui hata kidogo mambo ya magari ukiona gari ya 2004 hiyo bado ni mpya kwa hapa kwetu hata hizo unazoziona barabarani ni za miaka hiyo.....
Gari yangu carina Ti ni ya 1999 lakini hadi leo ipo poa kabisa na nimeshasafiri nayo DAR-MTWARA,DAR-MWANZA,DAR-ARUSHA bila shida yeyote njiani,siku nyingine uliza kwanza
 
Gari ya mwaka 2004 unaulizia kuhusu ubora wake? I mean hiyo gari ina miaka 15 sasa iweje iwe bora? Hapo kila kitu kimeshakwisha tayari.

Unaongelea hapo 2004 majuzi tu hapo,watu wanaendesha Vintage cars za 1960'a huko na yako fresh tu.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Unaongelea hapo 2004 majuzi tu hapo,watu wanaendesha Vintage cars za 1960'a huko na yako fresh tu.

Sent from my iPhone using JamiiForums

Unachanganya mambo, mleta Mada hajauliza kuhusu old timers, bali ameulizia Magari ya kawaida, na gari yenye umri wa 15 huwezi uliza ubora wake kwani kila kitu kwa kawaida kimeshakwisha.
 
Unachanganya mambo, mleta Mada hajauliza kuhusu old timers, bali ameulizia Magari ya kawaida, na gari yenye umri wa 15 huwezi uliza ubora wake kwani kila kitu kwa kawaida kimeshakwisha.

Na magari ya 1960's yaliyoko road ubora wake unasemaje?

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Back
Top Bottom