pingli-nywee
JF-Expert Member
- Sep 16, 2015
- 11,923
- 13,350
Baada ya muda mrefu hatimaye calendar ya mashindano ya riadha duniani imeanza tena. 'First leg' ya 2020 Diamond League(DL) ilianza kule Monaco, Ufaransa ijumaa hii.
Protokali zote mpya za COVID-19 zilizingatiwa, huku mashabiki 5,000 tu wakikubaliwa kwenye ukumbi wenye capacity ya watu 16,000.
Wanariadha wote walioshiriki na wasimamizi pia walilazimika kupimwa kabla ya hafla yenyewe. Wakenya waliibuka kidedea kwenye mbio zao, baada ya siku nyingi za mazoezi bila 'action'.
Bingwa wa dunia kwenye 5000m kwa wanawake Helen Obiri alistahimili ushindani mkubwa wa wahabeshi na akashinda kwa muda wa 14:22.12.
Naye bingwa wa dunia kwenye 1500m kwa wanawake Faith Kipyegon akaibuka mshindi kwenye mbio za 1000m na Timothy Cheruiyot akaibuka wa kwanza kwenye mbio za 1500m.
Obiri, Cheruiyot and Kipyegon shine at DL meet in Monaco