Riba ya 60% access Bank inatisha BOT mpo wapi?

Marire

JF-Expert Member
Joined
May 1, 2012
Posts
12,333
Reaction score
5,292
Heshima kwenu wakuu.
nimetoka kumdhamini jamaa yangu mkopo bank tajwa.
Hii riba haikubaliki Tanzania amekopa 5m rejesho 565,000 kwa mwezi mara miezi 12 .
Najiuliza bank kuu ya Tanzania haina viwango standard kwa mabank kabla ya kuwapa vibali?na je mbona Eura wameweza kukontrol bei ya nauli na mafuta? Bank kuu wanashidwa nini?
_Huyu kijana mwenzetu Naibu waziri wa fedha mwenye shahada ya uchumi daraja "A" hawezi kutusadia riba za mabank zishuke?
_ Naomba tujadili hili swala
 
MFI nyingi ni wanyonyaji sana.

Ulitaka BoT wafanyaje hapo?
 
26% ni kubwa sana ukilinganisha na wengine ambao huwa kati ya 17 hadi 22 kwa mikopo ya mtu mmoja mmoja!
 

Mkuu angalia Access Bank wasikuhold responsible kwa defamation. Check numbers zako vizuri kwani heading inasema riba ni 60% wakati tarakimu ulizotoa kwenye content zinapingana na hilo.
 
Mkuu angalia Access Bank wasikuhold responsible kwa defamation. Check numbers zako vizuri kwani heading inasema riba ni 60% wakati tarakimu ulizotoa kwenye content zinapingana na hilo.

mkuu ni 5%kwa mwezi ina maana kwa mwaka ni 60% majanga!
 
kwanza euwura hawajaweza control bei ya mafuta na naulu maana tangu vitu hivyo viwili vipande garama sijawahi sikiaa vikapunguaaaa garama
 
wakuu mbona hakuna aliyechangia kuhusiana na mada yangu? comments zenu ziko out of topic
 
wakuu mbona hakuna aliyechangia kuhusiana na mada yangu? comments zenu ziko out of topic

Mkuu wewe ndo umechanganya madesa! Mbona ukipiga hesabu inaleta 35.6% na siyo 60% kama unavyodai? Pamoja na hay bado riba ziko juu sana kwa nchi yetu. Sijui kwa nini hizi MFIs za private zinajiendea tu bila udhibiti! Hapa serikali ya ccm ndo ya kulaumiwa imeshindwa kusimamia Sera zake. Angalau NMB na CRDB wanajitahidi maana wako kati ya 13-19%. Kitakachotuokoa ni kuwatoa ccm madarakani ili tujaribu na wengine!!
 
mkuu ni 5%kwa mwezi ina maana kwa mwaka ni 60% majanga!

Hakuna kitu kama hicho. Kwa rejesho hilo riba si 60%. na benki onachaji 5% kwa mwezi. Angalia vizuri. Chukua 565,000 zidisha kwa 12 toa 5m. Hiyo tofauti ndiyo riba. Je hii ni adilimia ngspi ya Pxixt?
 
Sisi tunatoza aslimia 20 monthly.

Duh Mkuu Ndumba so hiyo ni 240% kwa mwaka that's killing kwa biashara ipi inayolipa kiasi hicho?

Anyway back to mtoa mada, kuna kitu hujakitaja kwenye hiyo 5% monthly ya Access Bank na kwa hilo hujawatendea haki. Kwamba hiyo rate ni at reducing balance kwa maana kwamba principal amount iko fixed kwa mwezi ila riba inapungua down the road kwani iko based on unpaid balance. Nasema hujawatendea haki Access Bank kwani najua zipo institutions ambazo rate zao c reducing balance based. So kama mdau mwingine alivyokokotoa hapo juu unapata kama 35% kwa mwaka ambayo si nzuri lakini pia si mbaya kama heading ya uzi inavyojaribu kutuaminisha.
 
TATIZO HAPA NI SHULE YA KI-FINANCE, NI KWELI 60% kwa mwaka, pia ni kweli 5 % kwa mwezi, PIA NI KWELI 35.6% YOTE NI MAJIBU SAHIHI TEGEMEA NA FORMULA YAKO
 
TATIZO HAPA NI SHULE YA KI-FINANCE, NI KWELI 60% kwa mwaka, pia ni kweli 5 % kwa mwezi, PIA NI KWELI 35.6% YOTE NI MAJIBU SAHIHI TEGEMEA NA FORMULA YAKO

asante kwa ufafanuzi maana kwa ilimu yetu ya madarasa sipo vyema sana kwa hesabu
 

Hapa ndio ninazidi kuchanganyikiwa. Kumbe Access Bank, NMB na CRDB ni MFIs? Nilijua Bank tajwa zinaitwa FIs tu na sio MFIs! Kweli Elimu haina mwisho!:doh:
 
TATIZO HAPA NI SHULE YA KI-FINANCE, NI KWELI 60% kwa mwaka, pia ni kweli 5 % kwa mwezi, PIA NI KWELI 35.6% YOTE NI MAJIBU SAHIHI TEGEMEA NA FORMULA YAKO

Mkuu kama uko vizuri kwenye mambo haya hebu tusaidie, kwa mfano mtu akikopeshwa 30m kwa riba ya 3% kwa mwezi at reducing balance, marejesho yake yatakuwaje kwa mwaka? Je! Hii riba ina unafuu wowote au ni mauaji? Mkopo unatakiwa urejeshwe ndani ya miezi 12. Hao ni Finca
 
Mtoa maada waja kulalamika jf huku ukimwancha mtu uliye mdhamini akijitwika hilo li mzigo? hili ni soko huria kabla ya kufanya maamuzi hebi jirizishe kwa shopping huenda ungefika nmb walau wao ni 18% lakini hii si ya total mkopo bali ya kila pesa bakia...pia ni wanyonyaji ingawa wanaunafuu flani hivi
 
Access bank wanakopoa kwenye commercial banks, sasa unategeme riba iwe kiasi gani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…